BRYSON MSHANA, TABORA
Mkoa wa wa Arusha umetwaa Ubingwa wa mchezo wa mpira wa Kikapu Wasichana, kwenye Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) yanayoendelea Mkoani Tabora.
Arusha imeibuka na ushindi baada ya kuifunga Pemba kwa Vikapu 34 – 10 katika mchezo wa kuvutia uliochezwa kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Tabora Wavulana Tarehe 12 Juni 2023, ukianza Saa 1:30 Asubuhi.
Kocha wa Timu ya Mkoa wa Arusha David Jalango, ameeleza kufurahishwa kwake na ushindi huo akisema ni matokeo ya wanafunzi wake kujituma na kuweka juhudi katika mchezo wa mpira wa kikapu hususan kwa wasichana.
“Wachezaji wamejituma sana tangu mchezo wa kwanza wa mashindano haya, timu zingine zilikuwa vizuri pia lakini tumeonesha kitu cha ziada na kushinda Ubingwa huu kwa ajili ya Mkoa wa Arusha” amesema Coach David
Kwa upande wake Kocha wa Timu ya Pemba Aboubakar Msabaha, amesema Arusha walicheza vizuri na walistahili ushindi na kuwapongeza wachezaji wake kwa mchezo wa kujituma japo hawajashinda Ubingwa.
“Arusha walicheza Vizuri, walituzidi katika maeneo mengi kiufundi na ni jambo la kawaida kwenye mchezo, sisi pia tulicheza vizuri lakini tulizidiwa na tumekosa ubingwa tutajipanga kwa wakati mwingine”
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…





