JUMA MOHAMED, MTWARA
mtwarapressclub@gmail.com
Wizara ya Uchukuzi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), wameunda kamati kwa ajili ya kushughulikia maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutaka Korosho za Mtwara zisafirishwe kupitia Bandari ya Mtwara.
Hayo yameelezwa Oktoba 04, 2023 Mkoani Mtwara na Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile, katika ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Bandari kujadili maandalizi ya kuhudumia zao la Korosho katika msimu wa 2023/2024.
Amesema kamati hiyo itaongozwa na mwenyekiti ambaye ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mhandisi Juma Kijavara, na kumuagiza “Kasimamie na tupate taarifa kwa haraka zaidi tuone maagizo haya ya Mhe. Rais yanafanyiwa kazi katika eneo letu.”
Aidha Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesema ndani ya mwezi huu wa Oktoba inatarajia kuiongezea Bandari ya Mtwara Kreni Mbili zenye uwezo wa kubeba Tani 160, ili kuiongezea ufanisi katika kuhudumia zao la Korosho.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mhandisi Juma Kijavara, wakati akiwasilisha salamu kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wadau wa Bandari, ikiwa ni maandalizi ya Bandari ya Mtwara kusafirisha zao la Korosho.
“Moja itatoka Bandari ya Tanga kuja hapa yenye uwezo wa kubeba Tani 100, na nyingine yenye uwezo wa kubeba Tani 60 itatoka Bandari ya Dar es Salaam kuja hapa.” Amesema Kijavara.
Hayo yanajiri ikiwa ni siku moja baada ya Wakuu wa Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma kukubaliana kutumia Bandari ya Mtwara kusafirisha Korosho zote zinazozlishwa katika mikoa hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas, alitoa tangazo hilo Oktoba 03, 2023 na wakatu wa ufunguzi wa kikao cha wadau wa soko la Korosho, kilichofanyika katika ukumbi Boma ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






