MWANDISHI WETU, ARUSHA

mtwarapressclub@gmail.com

Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Mohamed Mchengerwa Aprili 16, 2023 ametembelea makao makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), jijini Arusha lengo likiwa ni kujionea utekelezaji wa shughuli za Uhifadhi na Utalii. Katika ziara hiyo aliongozana na Katibu mkuu wa Maliasili na Utalii, Dkt Hassan Abbasi pamoja na Naibu Katibu mkuu, Anderson Mutatembwa.

Awali, akimkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Kamishna wa Uhifadhi – TANAPA, William Mwakilema, alimshukuru Waziri kwa kutenga muda na kuja kuzungumza na watumishi na kupongeza ushirikiano mkubwa ambao shirika limekuwa likipata kutoka  kwa viongozi wa Wizara ili kuifikia adhma ya serikali ya kufikia watalii millioni tano ifikapo 2025.

Aidha, Kamishna Mwakilema ameeleza hali ya mandeleo va miradi va kimkakati va kukuza utalii na kusema inaendelea vizuri ikiwemo miradi va miundombinu va malazi katika Hifadhi va Taifa Burigi -Chato na Kisiwa cha Rubondo pia miradi ya UVIKO -19  katika Hifadhi va Taifa

Serengeti, Tarangire, Kilimaniaro, Mkomazi, Saadani na Nyerere inayolenga kuboresha miundombinu ya malango ya kuingilia wageni, barabara, na viwanja vya ndege.

Baadhi ya wafanyakazi TANAPA wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii

Akizungumza na Watumishi hao, Waziri Mchengerwa aliwapongeza kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuhifadhi na kutangaza vivutio vyetu vya utalii na kuwataka kuongeza juhudi zaidi illi kufikia adhma ya serikali.

“Niwapogeze sana kwa kazi kubwa mnayoifanya katika kuhifadhi na kutangaza vivutio vyetu. Sisi kama viongozi wenu wa wizara idadi ya watalii millioni tano kwetu tunaiona ni ndogo sana nchi yetu ina vivutio vingi na maeneo ya kipekee tukiwa wamoja katika kutangaza idadi ya wageni nchini kwetu itaongezeka sana” amesema Mchengerwa

Pia, Mchengerwa ametoa rai kwa watumishi kuongeza nguvu zaidi katika kutangaza vivutio vyetu na kusisitiza mshikamano na nidhamu ya kijeshi na kubainisha

“ Tutambue taasisi yetu ni ya kijeshi ni vizuri tukitambua nidhamu ya kijeshi, wanajeshi hatuna kundi lingine sisi kama Jeshi tuna kundi moja tu la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” amesema Mchengerwa.

Waziri Mchegerwa amesistiza kufanya kazi kwa bidii na kuahidi ushirikiano na kusimama na watumishi kwa wakati wote na katika kila hali.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…