MWANDISHI WETU, MTWARA
Afisa Maendeleo ya Jamii wa shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania ( TPDC) ambaye pia ni Mratibu wa programu ya gasi mashuleni wa mikoa ya Lindi na Mtwara Oscar Mwakasege amesema wameanzisha klabu za gesi asilia mashuleni 17 kwa Mkoa wa Mtwara ili kuwajengea uelewa wanafunzi wa Shule hizo za sekondari waweze kuwa mabalozi wazuri wa rasilimali za gesi na mafuta.
Akizungumza wakati wa ziara ya wanafunzi 130 kutoka Shule Nane za Wilaya ya Mtwara iliyofanyika machi 09, 2023 Mwakasege amesema kuwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutambua rasilimali zilizopo nchini za nishati mafuta na gasi.
“Hawa wanafunzi wanatoka katika maeneo mbalimbali ya nchi ambapo tunapowaoa fursa kama hizi zinaweza kuwa chachu kwao katika kuzitunza na kuzisimamia rasilimali za nchi ambapo wametembelea kiwanda cha kuzalisha gasi asilia Mnazibay na kiwanda cha Kuchakata gasi asilia Madimba ili waweze kuijua gesi matumizi yake wajibu wao katika kuzilinda rasilimali hii muhimu Kwa taifa ambazo zimekuwa zikiliingizia taifa fedha na pia tukiwa wanufaika wa moja Kwa moja”


Kwa upande wake Meneja wa Kiwanda cha kuchakata gesi Madimba Mhandisi Sultan Pwaga amesema kwasasa wanachakata gesi asilia Futi za ujazo milioni 105 kiwango ambacho ni kikubwa ukilinganisha na awali ambapo tulikuwa tunazlisha Futi za ujazo milioni 45.
Amesema kuwa ziara ya wanafunzi hao kwao ni chachu ya kusoma Zaidi masomo ya sayansi ili waweze kuwa mabalozi wazuri wa kuzilinda na kuzitunza miundimbinu ya gesi asilia nchini.
“Hizi klabu ni kichocheo ambapo kinaweza kuwa msaada mkubwa kwa nchi kwakuwa Hawa ni kizazi kijacho ambapo tunawaelekeza kwakuwa tunafahamu kuwa ndio watabeba dhamana kubwa ya nchi ya kuendeleza miradi ya gesi asilia kwa mustakabali wa taifa tunaimani wakitambua dhamana kubwa waliyoanayo wanaweza kuwa msaada Kwa nchi na kuchukua nafasi katika miaka ijayo” ameeleza Mhandisi Pwaga
Kwa upande wake Daud Kasinje mwanafunzi wa Shule ya Sekondari naliendele amesema kuwa utolewaji wa elimu Kwa wanafunzi Kuna hamasisha sisi kusoma masomo ya sayansi ambayo wengi wanayaogopa.
“Gesi asilia ni gesi ambayo ni yetu ili kuzilinda rasilimali hii tunapaswa kuongeza bidii kusoma Zaidi na ili kuweza kuzisimamia miradi hii ambayo ni Faida kubwa Kwa nchi yetu kwanza inatengeneza umeme na kuongeza ajira Kwa nchi yetu hii inahamasisha kwa sisi wanafunzi kusoma masomo ya sayansi ili siku moja niweze kuwa sehemu ya watanzania wanaoweza kulinda na kusimamia rasilimali za nchi yetu” amesema Kasinje
Kwa upande wake Fatuma Suleiman mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mtwara Girls kidato cha Tano amekiri kujifunza mengi katika gasi kuanzia mnazi bay.
“Nimefurahi kuona kiwanda kikubwa kilichibeba dhamana kubwa ya nchi ya kuchakata gesi kikiwa na watanzania pekee wakiendesha mitambo na kuwezeshwa umeme kuzalishwa, matumizi ya majumbani Yaani furasa ni nyingi katika sekta ya gesi uwepo wa club hizi utaongeza Zaidi hamasa kwetu katika kusoma masomo hayo na kuwa na matamanio Zaidi ya kufanyakazi katikwa viwanda hivyo kwanza nimefurahi kuona Mhandisi wa kike imenipa moyo Zaidi”
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






