MWANDISHI WETU, MOROGORO

CHUO  Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kupitia Idara ya Sayansi ya Udongo na Jiolojia kimeshauri kuwa ni vema mkulima anayelenga kulima kwa tija kuhakikisha anapima afya ya udongo pamoja na afya ya mbegu atakazozitumia kabla ya kuanza shughuli za kilimo, ili kuepuka hasara na kuongeza ufanisi wa uzalishaji.

Hayo uameelezwa Mjini Morogoro tarehe 7 Agusti 2025, na Mtaalamu kutoka SUA Dkt. Hellen Kayagha  katika meonesha ya kilimo, uvuvuvi na ufugaji Kanda ya Mashiriki yanayofanyika katika viwanja vya naneane Manispaa ya Morogoro.

Dkt. Hellen Kayagha ameeleza kuwa Chuo hicho kinatoa huduma ya bure ya upimaji wa afya ya udongo, mimea na mbegu lengo ikiwa ni kuhakikisha wakulima nchini wanalima kisasa kwa kuzingatia kilimo chenye tija.

Amesema huduma hiyo inatolewa kwa wakulima na wageni mbalimbali wanaotembelea banda la SUA, ambapo sampuli zinapokelewa na majibu hutolewa ndani ya saa moja tu, hapo hapo bandani.

“Kwanini ni muhimu mkulima kupima udongo, kwa sababu inamsaidia kufahamu kiasi cha virutubisho kilichopo katika udongo na inampa uwezo wa kujua aina ya mbolea anayotakiwa kutumia na aina gani ya virutubisho ambavyo vinatakiwa kuongezwa kwenye udongo wake ili aweze kulima kwa tija na kupata mazao bora na yenye afya bora,” amesema Dkt. Kayagha.

Kwa upande wa mbegu, amesema mkulima anapoangalia afya ya mbegu anazotumia atakuwa na uhakika wa mbegu anayopanda inaota kwa kiasi gani shambani.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…