BRYSON MSHANA, MTWARA
mtwarapressclub@gmail.com
Viongozi na Wadau wa Elimu Mkoani Mtwara, wametakiwa kushirikiana na Uongozi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, ili kuhamasisha unasajli wa wasichana wengi waliokatisha masomo ya sekondari ukilinganisha na mwaka huu.


Akifungua mafunzo ya siku nne kwa walimu wa masomo ya sayansi wanaotokea katika vituo vya elimu ya watu wazima mikoa 14 nchini Tarehe 25 Aprili 2023 kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mtwara, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Hanaf Msabaha amesema mkoa wa Mtwara umefanikiwa kuandikisha wasichana72 katika vituo viwili vya sabasaba na Mangaka kwa mwaka wa masomo 2022/2023.
DC Msabaha ameeleza kuwa hali hiyo inaonesha kuwa idadi ni ndogo ukilinganisha na idadi ya wasichana walio katisha masomo, hivyo ni wajibu kwa wadau wa Elimu kushirikiana na uongozi wa Elimu ya watu wazima ili kuwafikia wasichana wengi zaidi katika mkoa.
Aidha Dc Msabaha amewasihi washiriki wa mafunzo hayo kushiriki kikamilifu na kuzingatia yote yatakayoelekezwa ili kuboresha ufundishaji wa masomo ya sayansi katika vituo vyao .
Ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kutooa elimu bila malipo, ikiwa sehemu ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya kitaifa na kimataifa ukiwemo maendeleo endelevu ya na Dira ya maendeleo ya mwaka 2020 /2025 yenye lengo la kumkomboa mtoto wa kike.
Naye Mratibu wa mradi SEQUIP kwa upande wa taasisi ya elimu ya watu wazima kitaifa wenye lengo la kuwarejesha watoto wakike waliokatisha masomo ya Elimu ya sekondari Baraka kionywaki, amesema mradi ulianza mwaka 2020 katika hatua ya uandaaji wa miongozo huku mwaka 2021/2022 ukiwa wa kwanza wa usajili ambao walifanikiwa kusaji wasichana 3,333 na mwaka 2023 wasichana 3,616 ambao wanaendelea na masomo.
Amesema kuwa malengo ya mafunzo hayo ni pamoja kuwajengea uwezo walimu wa masomo ya sayansi wanaofundisha kwenye vituo vya vinavyotekeeleza mradi huo, ukiwa na vituo 168 nchi nzima, na katika mkoa mtwara kumekuwa na vituo viwili vilivyo sajiliwa kwa elimu hiyo huku jumla ya wasichana 72 wakiwa tayari wameanza masomo.
Sambamba na hilo Bw. Baraka ametoa wito kwa jamii na viongozi mbalimbali mkoani Mtwara kutoa taarifa kwa wananchi juu ya fursa iliyotolewa na serikali ya watoto wa kike waliokatiza masomo kurejea na kuendelea na masomo.
Kwa upande wake Mwalimu Rehema Memba kutokea kituo cha kiwila sekondari wilaya Rungwe mkoani Mbeya, amesmea kupitia mafunzo hayo matarajio yao ni kupata ujuzi na uwezo mpya namna ya kuwawezesha ili kwanza wajikubali kuendena na mazingira yao na kujua namna ya kuahama kutoka hatua waliopo na kuelekea hatua nyingine waweze kujimudu kimaisha.
Pia Mwalimu Rehema amesema kuna uwezekano mkubwa wa wasichana hao kutimiza ndoto zao zilizokatishwa hapo awali kwani kumekuwa na msisitizo kutoka kwa viongozi aa serikali ambao wamekuwa wakiwatembelea katika vituo vyao na kutoa msaada wa kiutu pale unapohitajika .
Huu ni Mradi uliopo chini ya taasisi ya Elimu ya watu wazima kitaifa (SEQUIP) wenye lengo la kuwarejesha watoto wa kike waliokatisha masomo ya elimu ya sekondari kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kupata mimba,umabli mrefu na shule,magonjwa na hali duni ya maisha ulioanzishwa mwaka 2020/ 2021 chini ya taasisi ya Elimu ya Watu wazima kwa kushirikiana na Benk ya Dunia.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






