MUSA MTEPA, MTWARA
mtwarapressclub@gmail.com
Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara kimeendesha zoezi la uchangiaji wa damu lililojumuisha wadau mbalimbali wa Habari kutoka ndani na nje ya Mtwara, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 30 ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kimkoa Mei 6,2023.
Zoezi hilo lililofanyika viwanja vya Bima Manispaa ya Mtwara Mikindani, limeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Hanafi Msabaha ambaye amewapongeza waandishi wa habari katika mkoa wa Mtwara kupitia umoja wao, kwa uratibu mzuri wa zoezi hilo.
Zoezi linguine kama hilo limefanyiaka Wilayani Newala ambapo waandishi wa habari walijumuika na wadau wengine kuchangia damu katika Hospitali ya Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara.
“Niwapongeze waandishi wa habari kupitia chama chao pamoja na washiriki wao Ofisi ya damu salama kanda ya kusini na Chama cha msalaba Mwekundu Tanzania ofisi ya Mtwara kwa jambo hili kubwa na niombe liendelee katika maeneo mengine”
“Waandishi hawa wametuonyesha jambo lingine tofauti kabisa ambalo hatujazoea kuliona, wametuonyesha ushiriki wao wa kuchangia maendelea katika sekta ya Afya kwa vitendo, hakika sisi kama Serikali tumefurahi na tunawaahidi ushirikiano wakati wowote” ameeleza DC Msabaha
Katibu Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara Bryson Mshana amewashukuru wadau waliojitokeza kushiriki zoezi hilo, huku akieleza kuwa wanategemea kuliboresha na kuwa zoezi la kila mwaka.
” Mhe. Mkuu wa Wilaya lengo letu sio kuishia hapa, tunaenda kujipanga vizuri na wadau wetu ili kuanzia mwaka ujao 2024 zoezi hili lifanyike katika Wilaya zote za mkoa wa Mtwara kama sehemu ya Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ”
“Wote tumeshuhudia hamasa hii ambayo imewagusa mpaka wageni ambao wapo Mtwara kwa shughuli zingine lakini wameamua kushirikiana na sisi, hili ni jambo la heshima na linafaa kurndelezwa na kuwa la kudumu, nakuahidi Mhe . DC tutaliendeleza” amesisiza Mshana.
Kwa upande wake Meneja wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya Kusini, Dk Baraka Kandonga amesema katika Mkoa huo hali ya damu zipo lakini mahitaji kila siku bado yapo kwasababu kuna wagonjwa ambao wanahitaji damu na mapaka sasa awameshakusanya zaidi ya asilimia 98.
Baadhi ya wanahabari hao akiwemo Florence Sanawa wa gazeti la Mwananchi akiwa miongoni mwa wachagiaji wa damu ‘’ Nimejitolewa kuchangai damu ili kusaidia wale wenye uhitaji wa damu na damu inaokoa maisha ya Watu wengi sana kama vile watoto wachanga, akina mama wajawazito wakati wa kujifungua’’,
SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI USHIRIKI WA WADAU KATIKA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI
Na Munir Shemweta Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ushiriki wa wadau katika…






