MWANDISHI WETU, MTWARA

www.mtwarapressblog.co.tz

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), limesema uzalishaji wa gesi asilia katika kiwanda cha kuchakata gesi hiyo cha Madimba Mkoani Mtwara, umeongezeka kutoka futi za ujazo 45 mwaka 2015, hadi kufikia futi za ujazo 105.

Hayo yameelezwa kiwandani hapo Machi 9, 2023 na meneja uzalishaji wa kiwanda hicho Mhandisi Sultan Pwaga, wakati wa ziara ya Wanafunzi wa klabu za gesi na mafuta kutoka baadhi ya shule za sekondari za Wilayani Mtwara.

Amesema uzalishaji huo unatarajiwa kuongezeka baada ya kukamilika kwa mradi wa bomba la Gesi kutoka visima vya Ntolya kata ya Nanguruwe hadi kiwandani hapo, lenye urefu wa kilometa 25.

“Na kazi hiyo tunatarajia itakamilika mwishoni mwa mwaka huu au mwanzoni mwa mwaka 2024, kwahiyo mchango wake wa gesi katika uchumi wa umeme pamoja na viwanda tunatumaini utaongezeka mara dufu.” Amesema Mhandisi Sultan Pwaga.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…