MWANDISHI WETU, TABORA

mtwarapressclub@gmail.com

Wakulima wa zao la Karanga  katika Wilaya za Uyui na Urambo Mkoani Tabora wameridhishwa na tafiti shirikishi zinazotolewa kwao na watafiti wa zao hilo kutoka Tasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania Tari  Kituo cha Naliendele Mtwara kupitia mashamba darasa yaliyoanzishwa na kituo hicho katika kata hiyo.

Akizungumzia ushirikishwaji huo hivi karibuni Tabu Ramadhan ambaye Mkulima wa zao la Karanga Kata ya Nsimbo Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora amesema kuwa shamba darasa hilo limekuwa msaada mkubwa kwao kwakuwa wamepata elimu ambayo awali hawakuwa nayo.

Amesema kuwa mbegu bora ni nzuri zinafaa kwa kilimo biashara kwakuwa zina mavuno mengi ambapo ukivuna unakuta shina moja lina karanga 200 haya kwetu ni mafanikio makubwa.

“Tunaiona tofauti kubwa kati ya mbegu za asili na mbegu bora haya ndio manufaa ya teknolojia mkulima analima katika eneo dogo lakini anapata mavuno mengi”

“Mbegu bora zinazaa karanga kubwa nzito lakini za asili ni ndogo sana ujio wa mbegu hizi utaongeza hamasa zaidi kwa wakulima kulima zao la karanga katika mkoa huo”

Nae Zubella Juma mkulima wa zao la karanga kijiji cha Kazimoto ameeleza kuwa wamepata elimu sahihi ya kulima zao la karanga sasa tumeacha kulima kwa kutumia matuta.

“Ukilima kwa matuta ukivuna unapata gunia 1-2  lakini ukilima bila matuta unaweza kupata magunia zaidi ya 5 hivyo kusaidia wakulima kuboresha maisha yetu kwakuwa tunaweza kuongeza thamani pia kwaongeza kipato zaidi” amesema Juma

Ernesta Buretta Ofisa Kilimo Kata ya Nsimbo  Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora amesema kata hiyo bado haijawa na wakulima wakubwa wa zao hilo.

“Katika kata yetu japo tunajaribu kuhamamsha wakulima waone zao la karanga kama fursa kwao kwakuwa wakazi wengi wa kata hii ni wakulima sio wafanyakazi hivyo wakiitikia wanaweza kuongeza uzalishaji wa  karanga na kuongeza kipato cha mkulima na vijiji kwa ujumla”

Nae Afisa Kilimo wa Kata ya Itundi Wilayani Urambo Mkoani Tabora Ramadhani Changiki amesema kuwa utafiti shirikishi umeonyesha njia kwa wakulima wa kata hii ambapo tunaamini kuwa uzalishaji utaongezeka zaidi kwa siku zijazo.

“Kwakweli mbegu bora imeongeza mavuno  tofatui na mbegu ya zamani hii itatoa fursa zaidi kwa wakulima kulima zao hilo ambalo limewezesha wakulima kupata elimu kupitia mshamba darasa yenye tija kwa jamii” amesema Changiki

Hata hivyo Mtafiti wa zao la Karanga kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania TARI kituo cha Naliendele Juma Mfaume anasema kuwa utafiti shirikishi umeleta mafanikio makubwa kwa wakulima wa zao la karanga.

“Utafiti huu tumefanya katika mikoa mbalimbali ambayo zao hili linafanya vizuri na kubaini kuwa mbegu hizi bora zina faa na baadhi zinauwezo sana kwa baadhi ya maeneo ndio maana tukaanza kufanya utafiti shirikishi kwa kusaidiana na wakulima” ammeleza Mfaume

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…