BRYSON MSHANA, TABORA
Michezo ya wanafunzi wa Shule za Mshingi Tanzania (UMITASHUMTA) imeingia siku ya pili Katika mji wa Tabora Mkoani Tabora, huku michezo mbalimbali ikiendelea kuchezwa.
Katika michezo iliyochezwa mapema Saa 2 asubuhi ya tarehe 04 Juni 2023, Timu za soka kwa wasichana kutoka Mikoa ya Mtwara na Pwani zilikutana katika Uwanja A Shule ya Sekondari Tabora wavulana.
Mchezo huo wa kuvutia uliisha kwa Mkoa wa Pwani kuibuka na ushindi bada ya kuifunga Mtwara kwa gili 1-0, goli lililofungwa katik kipindi cha kwanza.
Aidha upande wampira wa wavu kwa wavula ulizikutanisha Mikoa ya Pwani na Katavi, matokeo yakiwa ni ushindi wa Pwani seti 3 na Katavi 1.
Kwenye mpira wa wavu wasichana, Mkoa wa Lindi uliibuka na ushindi baada ya kuwashinda Shinyanga kwa seti 3-1
Mashindano ya UMITASHUMTA 2023 ambayo yanahusisha michezo mbalimbali yalianza Juni 03, 2023 na kushuhudiwa na Naibu Katibu mkuu anayeshughulikia Elimu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), Dr. Charles Msonde.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






