MWANDISHI WETU

Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania UMITASHUMTA na yale ya Shule za Sekondari UMISSETA kwa mwaka 2025 yanatarajiwa kufanyika Mkoani Iringa kuanzia Juni 7,2025.

Mashindano hayo yatajumuisha wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar, yakihusisha michezo mbalimbali kama soka kwa wavulana na Wasichana,Mpira wa kikapu, Netiboli,Wavu na Riadha.

Michezo mingine ni mpira wa Goli ambao ni maalum kwa ajili ya wanafunzi wenye uono hafifu, pamoja na Sanaa za Michezo na Burudani ambayo inahusisha ngoma za asili, kwaya na Muziki wa Kizazi kipya (Bongo Flavor).

Mashindano hayo pia yatajumuisha michezo mingine kwa wanafunzi wenye ulemavu, ikiwepo soka Wasichana na Wavulana pamoja na Riadha.

Bryson Mshana ni mmoja wa waandishi rasmi wa habari za mashindano hayo kutoka Team ya Habari ya OR-TAMISEMI , ambaye ushiriki wake wa miaka mitatu mfululizo, umemfanya apate uzoefu mkubwawa kuyafahamu na kuyaelezea kwa kina zikiwepo faida zake kwa wanamichwzo na Taifa kwa Ujumla.

Endelea kufuatilia zaidi kupitia zaidi juu ya kile kilichojiri katika mashindano ya UMITASHUMTA & UMISSETA 2024 koani Tabora https://youtu.be/LroEdFsb95g?si=JnxVR4aGyrnnACMp

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…