BRYSON MSHANA, MTWARA
Mamlaka ya Bandari Tanzania – TPA, imeahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina yake na waandishi wa habari Mkoani Mtwara, ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwashirikisha katika shughuli mbalimbali zinazoandaliwa na Bandari ya Mtwara.
Afisa Uhusiano Mkuu wa TPA Levina Kato, ametoa ahadi hiyo Novemba 21, 2023 wakati akizungumza katika siku ya pili ya Jukwaa la Habari na Mawasiliano mkoa wa Mtwara, linaloendelea Mjini Mtwara, likilenga kuwaunganisha wadau kutoka vyombo vya habari, maafisa habari na wakuu wa Taasisi mbalimbali za Serikali.
Bi. Levina alikuwa akiwasilisha mada kuhusu Mamlaka ya Bandari Tanzania na majukumu yake, ambayo ililenga kuwajengea uelewa washiriki wa jukwaa hilo kuzifahamu kazi na majukumu ya TPA.
“Tumekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na waandishi wa habari wa Mtwara na tutaendelea kuwashirikisha katika shughuli zetu kulingana na taratibu zitakazokuwa zimewekwa na Taasisi kulingana na shughuli husika kwa lengo la kuhakikisha kuwa kila chombo cha habari kinafikiwa”
“Hatuwezi kuwashirikisha waandishi wote katika kila tukio, kwa sababu pia za kibajeti, lakini niwahakikishie kuwa kila watakapohitajika waandishi watajulishwa ili kushiriki katika shughuli zetu mbalimbali”
“Pia kupitia Klabu yenu ya waandishi wa habari, nichukue nafasi hii kuwakaribisha kutembelea Bandari ya Dar es salaam ili kujionea shughuli mbalimbali zinazoendelea huko na kuwajulisha wananchi kupitia vyombo vyenu vya habari” amesema….
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano Bandari ya Mtwara Bw. Faraji Mbulalina, ameeleza kuwa wamekuwa wakishirikisha waandishi wa habari katika kila shughuli inayofanyika Bandandrini inayohitaji waandishi wa habari, na wataendelea kufanya hivyo katika siku zijazo.
“Tumekuwa tukihakikisha kuwa kila kazi inayohitaji waandishi wa habari katika Bandari ya Mtwara tunafanya hivyo, ni niwaahidi kuwa tutaendelea kushirikiana kwa kuzingatia miongozo tuliyoiweka na tunayoendelea nayo”
TPA ni wadhamini rasmi wa Jukwaa la Habari na Mawasiliano Mkoa wa Mtwara, lililozinduliwa Novemba 20, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas na linatarajiwa kufanyika kila mwaka.
Katika uzinduzi huo, Kanali Abbas alisisitiza juu ya Taasisi za Serikali kushirikiana na vyombo vya habari, ili kuviwezesha kuandika habari mbalimbali za maendeleo na miradi inayoendelea kutekelezwa na Serikali katika mkoa wa Mtwara.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






