TFS – KANDA YA KUSINI
Wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS kupitia Hifadhi ya Shamba la Miti Rondo Halmashauri ya Wilaya ya Mtama mkoani Lindi, wamesherehekea siku ya Mazingira Duniani kwa kupanda miti 100 aina ya Misindano, pamoja na kugawa Vifaa vya michezo kwa Vijiji vinavyozunguka hifadhi hiyo.
Afisa Uhifadhi muandamizi wa TFS Hifadhi ya Shamba la Miti Rondo, Samson Mweta amesema, Vifaa walivyogawa Juni 5, 2023 ni pamoja na Jezi, Mipira na Filimbi kwa timu za Mpira wa miguu na mikono zilizopo ndani ya Vijiji Vinne vinavyozunguka Hifadhi hiyo.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Shaibu Mchinga ambae ndiye Mgeni rasmi, kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo hilo Nape Nnauye, amewaomba Wananchi wanaozunguka Hifadhi hiyo hasa Vijana, kuwa Mabalozi wazuri katika kuulinda msitu huo kwa sababu una umuhimu mkubwa sio tu kwa wakazi hao, bali hata Taifa kwa ujumla.
Vifaa hivyo ambavyo ni Jezi, Mipira na Filimbi vina thamani ya Shilingi milioni tatu (3,000,000/=) na ni sehemu ya utekelezaji wa shughuli za TFS katika kuimarisha ushirikiano na vijiji vinavyozunguka Hifadhi ya Shamba la Miti Rondo
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






