KWA HISANI YA BBC
mtwarapressclub@gmail.com
Klabu ya Crystal Palace ya nchinbi Uingereza, wanapanga kujariu kumsajili mchezaji huru wa Ubelgiji Eden Hazard kwa kumpa mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea na Real Madrid mweye umri wa miaka 32, mkataba wa mwaka mmoja huko Selhurst Park licha ya majeraha yake. (Football TransferS)
Brentford wameweka bei ya pauni milioni 80 kwa mshambuliaji wa Uingereza Ivan Toney, 27, huku Arsenal na Tottenham zikiwa na nia ya kumsajili mchezaji huyo mwezi Januari mara baada ya kutumikia marufuku yake ya miezi minane kwa kukiuka sheria za kucheza kamari. (tIMES – usajili unahitajika)
Arsenal wanakaribia kufikia makubaliano na Real Sociedad kuhusu mkopo wa msimu mzima kwa beki Kieran Tierney, 26. (The Athletic – Usajili unahitajika)
The Gunners wameafikiana na Monaco ada ya euro milioni 45 (£38.6m) pamoja na nyongeza kwa mauzo ya mshambuliaji wa Marekani Folarin Balogun, 22. (RMC Sport – kwa Kifaransa)
Manchester United wanakaribia kufikia kandarasi ya mwaka mmoja na Jonny Evans, 35, katika hatua ambayo inaweza kuibua shaka juu ya mustakabali wa beki mwenza Harry Maguire, 30, Old Trafford. (Telegraph – usajili unahitajika)
Klabu ya Albania ambayo haikutajwa jina ina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Mason Greenwood, 21, baada mchezaji huyo na United kufikia uamuzi wa kuondoka Old Trafford baada ya uchunguzi wa ndani. (Talksport)
Tottenham wanavutana na Nottingham Forest kuhusu ada ya kumsajili Brennan Johnson, huku klabu hiyo ya East Midlands ikionyesha kuwa haiko tayari kumruhusu mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kuondoka kwa kitita cha pauni milioni 40. (Standard)
Chelsea pia wana nia ya kumsajili Johnson na mchezaji huyo anafikiriwa sana Stamford Bridge. (Football London)
Fulham wamemchunguza beki wa Uingereza , 29, kwa lengo la kumsajili kutoka Tottenham baada ya kiungo huyo kuachwa nje ya kikosi cha mkufunzi wa Spurs Ange Postecoglou kwa mechi mbili za kwanza za Ligi ya Primia. (Sky Sports)
Manchester City wanajiandaa kuwasilisha ofa ya pili kwa Wolves kumnunua kiungo wa kati wa Ureno Matheus Nunes, 24, baada ya dau la kwanza la takriban pauni milioni 47 kukataliwa. (Telegraph – usajili unahitajika)
Lakini City wako tayari kuachana na dili la Nunes ikiwa hawaamini kuwa litawapa thamani ya pesa. (Standard)
Barcelona watamsajili Joao Cancelo kwa mkopo wa msimu mzima kutoka Manchester City siku chache zijazo lakini hakutakuwa na chaguo la kumnunua beki huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 29 aliyejumuishwa kwenye mkataba huo. (Marca kwa Kihispania)
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






