BRYSON MSHANA, MTWARA

mtwarapressclub@gmail.com

Dunia inakabiliwa na mabadiliko ya tabia nchi na uchafuzi wa mazingira ambayo tayari yameanza kuleta athari hasi kwa binadamu, wanyama na viumbe hai waishio majini ikiwemo Samaki katika maeneo mbalimbali ulimwenguni.

Lengo namba 14 la Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs) linazungumzia Maisha ya viumbe hai waishio chini ya maji na kusisitiza matumizi endelevu na uhifadhi wa rasilimali zilizopo baharini ifikapo mwaka 2030.

Kwa upande wake Umoja wa Mataifa umekuwa ukisisitiza nchi wanachama kuhakikisha wanadhibiti aina zote za uchafuzi ikiwa ni pamoja na taka za plastiki zinazotupwa maeneo ya Bahari, Ziwa na Mito ili kulinda mifumo ya ikolojia na kuepusha athari mbaya kwa viumbe hai.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Zaidi ya tani milioni 400 za plastiki huzalishwa kila mwaka kote duniani, nusu ya taka hizo hutumika tu mara moja, Kati ya hizo, chini ya asilimia 10 ya plastiki huchakatwa, na kila mwaka takriban tani kati ya milioni 19 na milioni 23 huelekea kwenye Maziwa, Mito na Bahari.

Ili kulinda maisha ya binadamu pamoja na viumbe hai waishio chini ya maji hapa nchini Tanzania, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania – TASAC limeeleza kuwa linaendelea kuchukua hatua kuhakikisha kuwa meli zinazotumia mito, maziwa na bahari zinafuata kanuni za utunzaji wa mazingira.

Bi. Leticia Mutaki ni Mkurugenzi wa udhibiti wa ulinzi usalama wa vyombo vya Maji Baharini pamoja na utunzaji wa mazingira ya bahari kutoka TASAC ambaye anasema kuwa wanaendelea kuwakumbusha wadau wao juu ya kuzingatia utunzaji wa mazingira wanapukuwa wanatumia bahari.

“Usalama wa majini ni jukumu letu kuu, tunafuatilia meli zote zinzazofanya safari na shughuli nyingine kwenye maeneo ya Bahari, Mito na maziwa ili kuhakikisha kuwa shughuli hizo haziathiri mazingira na kuhatarisha uhai wa viumbe vilivyopo”

“ wakati mwingine Meli zinaweza kumwaga mafuta baharini au kutupa taka zingine huko, tumeweka sheria kali ili kuzuia hali hiyo na pale inapobainika kuna uvunjifu wa sheria basi hatua stahiki zinachukuliwa, lengo letu ni kuhakikisha kuwa mazingira ya bahari yanakuwa salama wakati wote kwa ajili ya usatawi wa watumiaji wengine na ukuwaji wa viumbe hai waishio baharini”

“Tunafuatilia meli zisimwage uchafu, mafuta baharini lakini pia tunaangalia hata meli ambazo zinaweza zikafanya vitendo vyovyote vile kinyume na sheria hivyo kama kuna meli tutaiona kutokana na kubaini kuwa haifuati utaratibu tunachukua hatua kwa kushirikiana na vyombo vyetu vingine vya serikali.’’ amesema Bi. Leticia Mutaki

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…