MWANDISHI WETU, MTWARA
mtwarapressclub@gmail.com
Naibu Waziri wa wizara ya nishati, Judith Kapinga amelihimiza Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania – TANESCO kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha mikoa ya Mtwara na Lindi inapata umeme wa kutosha.
Naibu Waziri Kapinga ameyasema hayo tarehe 14/09/2023 wakati alipotembelea Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa kutumia Gesi Asilia cha Mtwara.
Kituo hicho chenye mitambo 13 yenye uwezo wa kuzalisha umeme Megawati 30.4, kwa sasa kinazalisha Mwgawati 19 kutokana na mitambo mitatu kuwa katika Matengenezo hali ambayo imesababisha upatikanaji wa umeme kusuasusa katika baadhi ya maeneo yanayohudumiwa na kituo hicho.
Naibu Waziri amefanya ziara katika kituo hicho ili kuangalia halisi hali ya mitambo na uzalishaji wa umeme ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa hali ya upatikanaji wa huduma ya umeme kwa wananchi wa mikoa ya Mtwara na Lindi.
Amemuelekeza Meneja wa Kituo hicho kinachozalisha Umeme kwa kutumia Gesi Asilia, kuhakikisha wanafanya jitihada za kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme mkoani humo ili kukidhi hamu ya wakazi wa mikoa ya Mtwara na Lindi.
Akizungumza kwa niaba ya Watumishi wa Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa kutumia Gesi Asilia cha Mtwara, Meneja wa Kituo hicho, Mtoba Kasika Biseko, ameahidi kuwa, watafanya kazi kwa moyo wa kujituma.
Katika ziara hiyo, Naibu Waziri wa Nishati, aliambatana na Kamishna wa Umeme wa Wizara ya Nishati, Innocent Luoga, Naibu Mkurugenzi, Usambazaji Umeme wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania – TANESCO Athanasius Nangali na Meneja TANESCO Mkoa wa Mtwara Mha. Tawakali Rwahila.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






