BRYSON MSHANA, MTWARA
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Mkoa wa Mtwara, imesaidia kufanikisha kupatikana kwa malipo ya wakulima wa Korosho msimu 2024/2025 ambayo yalikuwa yamekwamishwa na viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika.
Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa leo tarehe 27 Mei 2025 na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mtwara Elisante Mashauri, kiasi cha fedha shilingi 79,837,568 ambazo ni fedha za wakulima wa korosho walizokuwa wanadai katika msimu 2024/2025 zililipwa katika kipindi cha Januari hadi machi 2025.
“kutokana na elimu iliyotolewa kwa wananchi, wamejenga ujasiri na kuwawezesha kutoa taarifa za vitendo vya rushwa na ubadhirifu, ikiwepo taarifa za vitendo vya rushwa na ubadhirifu wa fedha za wakulima wa Korosho katika vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS)” amesema Mashauri.
Katika hatua nyingine TAKUKURU imefanya ufuatiliaji wa rasilimali za umma kwa kukagua miradi ya maendeleo 13 yenye thamani ya aidi ya shilingi Bilioni 7 katika sekta ya Afya, Miundombinu na Elimu ili kubaini viashiria vinavyoweza kusababisha upotevu wa fedha za umma.
Taarifa ya TAKUKURU imeeleza kuwa itaendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali kupitia mikutano, semina, vipindi vya Redio, maonesho na Klabu za wapinga rushwa ili kuzidishi kufikisha ujumbe wa kuzuia na kupambana na rushwa kwa jamii.
SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI USHIRIKI WA WADAU KATIKA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI
Na Munir Shemweta Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ushiriki wa wadau katika…






