BRYSON MSHANA, TABORA

mtwarapressclub@gmail.com

SERIKALI ya awamu ya Sita imefanya jitihada kubwa katika kuendelea kuimarisha na kuboresha michezo katika shule za msingi na Sekondari nchini pamoja na vyuo vya ualimu nchini

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Angellah Kairuki leo Juni 6, 2023 wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) na Umoja wa Michezo na Taaluma kwa wanafunzi wa shule za Sekondari (UMISSETA) uliofanyika mkoani Tabora.

Amesema Serikali imeendea kuhakikisha fedha kwa ajili ya michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA na kuboresha miundombinu ya michezo kwa ajili ya shule mbalimbali za msingi na sekondari ili kuweka mazingira mazuri ya kufanyia michezo nchini

Waziri Kairuki anaendelea kufafanua kuwa Serikali imeshatambua shule takribani 56 ambazo zitatumika kama  vituo vya michezo katika Mikoa  kwa ajili ya kuwandaa wanamichezo  pamoja na  wataalam mahiri wa michezo

Ameongeza kuwa kupitia Ofisi ya Rais Utumishi  serikali imeendelea  kuwabadilishia Miundo ya Utumishi walimu wa michezo na waliosomea sanaa na utamaduni ili kuwa Maafisa Michezo na Maafisa Utamaduni katika Mamlaka za Serikali za mitaa.

Aidha, amesema Serikali imeandaa mwongozo wa uendeshaji wa michezo ya UMITASHUMTA, UMISSETA na FEASSSA na kuweka taratibu zinazopaswa kuzingatiwa katika uendeshaji wa mashindano ya michezo kwa shule za msingi na sekondari kuanzia ngazi ya shule hadi Taifa na ushiriki wa Tanzania katika mashindano ya michezo ya wanafunzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (FEASSSA).

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…