BRYSON MSHANA, MTWARA

 mtwarapressclub@gmail.com

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas, amewataka wananchi wa mkoa huo kuendelea kuchua tahadhari ya mvua za Elnino kama ambavyo imetolewa na mamlka ya hali ya hewa nchini, ili kuepusha madhaya yanayoweza kusababishwa na mvua hizo.

Kanali Abbas amesema hayo Mjini Mtwara Disemba 23, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake, ikiwa na sehemu ya kuwatakia heri ya sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya 2024 wananchi wa Mkoa wa Mtwara.

Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa salam zake za heri ya sikukuu kwa wananchi zinaenda sambamba na kuwaomba kuchukua tahadhari katika maeneo mbalimbali ikiwepo kwenye makaazi yao, ili kuepuka madhara iwapo kutakuwa na mvua za kuzidi wastani.

“Tumejitahidi kuchukua tahadhari katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu, lakini bado hilo halitoshi lazima tuwatahadharishe wananchi wetu kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na wale wanaoishi maeneo yanayojaa maji kuondoka na kuhamia maeneo ya miinuko iwapo wataona hali inakuwa tofauti”

“Kwa Manispaa lipo eneo Korofi la Mtaa wa Kiyangu ambalo timu ya wataalmu imeendelea kulishughulikia, lakini yapo maeneo mengine kule Nanyamba na Nanyumbu ambayo yapo jirani na Mto Ruvuma, tumeshawafikia wananchi kuwapa elimu na tunaendelea kufanya hivyo hususan wakati huu wa msimu wa mvua” ameeleza Kanali Abbas.

Kuhusu hali ya Usalama, Kanali Abbas amesema kuwa Mkoa uko shwari na vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea na kazi zake kama kawaida, huku akiwataka wananchi kuendelea kutii sheria za nchi bila shuruti wakati wote wa shamrashamra za sikukuu za mwisho wa mwaka.

Amewasihi watumiaji wa barabara na vyombo vya usafiri katika maeneo mbalimbali ya Mkoa, kuzingatia sheria za usalama barabarani, ili kuepesha ajali ambazo zinaweza kugaharimu maisha ya watuau kuwasababishia wengine ulemavu.

“Hali ya usalama ni nzuri, mkoa wetu una usalama wa kutosha lakini niendelee kuwasisitiza watumiaji wa barabara wakiwepo wenye vyombo lakini pia watembea kwa miguu wote kwa pamoja wajitahidi kuzingatia na kufuata sheria ili tumalize sikukuu hizi salama” ameongeza Kanali Abbas.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…