MWANDISHI WETU, MTWARA
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbasi ameridhishwa na ubunifu mkubwa ulionyeshwa na wananafunzi wa Shule mbalimbali Msingi na Sekondari mkoani hapa.
Mkuu wa mkoa amesema hayo machi 15, 2023 baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya Elimu kwa lengo la kukagua na kuona shughuli mbalimbali za elimu zikiwemo dhana za kufundishia na kujifunzia.
Kanali Ahmed Abbasi pia amejionea ubunifu wa nyenzo mbalimbali zilizotengezwa na wanafunzi kwa kutumia teknolojia ya kisasa na wezeshi kwa matumizi ya wananchi wawapo majumbani , mashambani na kwenye sehemu za kazi.
Akizungumza katika maonyesho hayo amesema kuwa ameridhishwa na ubunifu hizo zinazoonyesha kuwa walimu wanafanya kazi kubwa ili kuweza kuinua elimu katika mkoa huu.
“Hili tukio ni kubwa na muhimu kwa taifa tunaona namna Rais Samia Suluhu anavyopambania elimu katika nchi hii naona utayari na tumedhamilia kufanya mambo makubwa na kufanya muendelezo kwa mkoa kukuza sekta ya elimu katika kuongeza molali ya wanafunzi na walimu jitihada kubwa zinafanyika tunaona niwapongeze wadau wote” amesema Kanal Abbas
Afisa Elimu Msingi Halmashauri Mji Masasi Hamida Msemo amesema kuwa wamejipanga katika kutengeneza dhana za kutosha na kuwashirikisha watoto katika michezo mbalimbali za kufundishia KKK ili waweze kumaliza darasa la saba wakiwa wanajua kusoma na kuandika.
“Unajua ipo tabia ya wazazi kuwahimiza watoto wao wasifanye vizuri katika matokeo yao ya darasa la saba kwenda kidato cha kwanza tunajaribu kuwa elimu ili kuweza kuwaeleza namna bora ya kuona umuhimu wa watoto hao kusoma na kuwa na elimu kubwa” amesema Msemo

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…