BRYSON MSHANA, LINDI
mtwarapressclub@gmail.com
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas, amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia suluhu Hassan anatambua umuhimu wa Kilimo endelevu nchini ndio maana mekuwa akitoa fedha kwa taasisi za utafiti wa kilimo Nchini.
Kanal Abbas ametoa kauli hiyo Agusti 06, 2023 kwenye maonesho ya Mbegu za Asili Kanda ya Kusini 2023, yaliyoandaliwa na Shirika la SWISSAID Tanzania kwenye viwanja vya maeonesho ya Wakulima na wafugaji Nanenane eneo la Ngongo Manispaa ya Lindi Mkoani Lindi.
“Niwapongeze waandaaji wa tukio hili, Haya ni maonesho muhimu sana kwa sekta ya kilimo, hata Rais wetu Dkt. Samia anatambua umuhimu wa kukuza kilimo kwa na mbegu za asili, ndio maana amekuwa akitoa fedha nyingi kwenda kwenye taasisi zetu za utafiti wa mbegu nchini, ili kuimarisha sekta ya kilimo” ameeleza Kanali Ahamed.
Ameeleza kuwa Serikali inathamini mchango wa SWISSAID Tanzania na washirikia wake walioandaa maonesho Mbegu za Asili, kwani yanalenga kuhamasisha matumizi ya mbegu na vyakula vya asili kwa ustawi wa Taifa la Tanzania.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa SWISSAID Tanzania Bi. Betty Malaki, ameeleza kuwa Shirika hilo limekuwa likipata ushirikiano kutoka kwa Serikali na wadau wengine nchini, jambo ambalo linaonesha dhamira ya dhati iliyopo katika kuhamsisha matumizi ya mbegu na vyakula vya asili.
Betty amesema kuwa juhudi za shirika hilo zinalenga kuboresha uchumi wa wananchi kupitia kilimo hai, lakini pia kuzidi kuhamasiha juu ya ulaji wa vyakula vya asili kwa ajili ya Afya bora.
Nao wananchi mbalimbali kutoka mikoa ya Lindi na mtwara ambao wamenufaika na program mbalimbali za SWISSAID Tanzania, wameeleza kuwa upo utofauti mkubwa wanaouona wakilinganisha na kabla hawajaanza matumizi mbegu na vyakula vya asili.
Victoria Mchowe kutoka Kikundi cha Muungano kilichopo Kijiji cha Nangose Masasi, na Tausi Mwachi kutoka kikundi cha Upendo kilichopo Kijiji cha Nyengedi-mtwama Lindi, wamesema muamko wa wananchi kutumia vyakula vya asili umekuwa ukiongezeka.
“Sisi tunazalisha, tunatunza na kuuza Mbegu pamoja na Vyakula vya Asili, uhitaji ni mkubwa kutokana na wateja mbalimbali kuhamasika katika masuala haya ya kilimo hai jambo ambalo linatuwezesha kupata kipayo na kuendesha maisha yetu” Victoria Machowe
Afisa Miradi Mwandamizi wa SWISSAID Tanzania Bi Veronica Masawe amesema kuwa uwepo wao katika mapnesho ya Nanennane umesaidia kuahamasisha matumizi ya Mbegu na vyakula vya sili katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya kusini.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






