BRYSON MSHANA, TABORA

mtwarapressclub@gmail.com

Mikoa ya Pwani na Manyara imeng’ara kwenye fainali baada ya kuibuka mabingwa wa riadha mita 100 na 1,500 wasichana na wavulana katika Mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA 2023) Mkoani Tabora.

Fainali ya kwanza ya riadha UMISSETA 2023 imefanyika Leo Asubuhi Tarehe 19 Juni 2023 kwenye viwanja vya shule ya Sekondanri Wavulana Tabora, na katika Mita 1,500 Wasichana Salma Charles wa Pwani kuibuka mshindi baada ya kutumia dakika 4.42.31 akifuatiwa na Zahara Ramadhani wa Singida aliyetumia dakika 4.42.97, na nafasi ya tatu kwenda kwa Evalina Mwampashi wa Songwe dakika 4.54.3.

Mita 1,500 Wavulana Agustino Lenald aliupa mkoa wa Manyara ubingwa baada ya ya kukimbia kwa dakika 3.55.97, akifuatiwa na Joseph Gewe pia wa Manyara aliyetumia dakika 4.04.43 na Damian Christian wa Arusha 4.04.94.

Upande wa Riadha Mita 100 Wasichana, Mkoa wa Pwani uliibuka tena na ushindi baada ya Siwema Julius kukimbia kwa sekunde 0.12.66 akifuatiwa na Stumai Msekwa wa Njombe Sekunde 0.12.72 na Bertha Adrea wa Kilimanjaro akamaliza nafasi ya tatu akitumi Sekunde 0.13.03.

Riadha Wavulana Mita 100 Ubingwa umeenda Mkoa wa Shinyanga baada ya Makoye Kasuka kutumia Sekunde 0.11.22, Dodoma ikashika nafasi ya pili kufuatia Baraka Nsajigwa kukimbia kwa Sekunde 0.11.35 na Matiko Nyamalaga wa Mkoa wa Mara kumaliza watatu kwa Sekunde 0.11.38.

Fainali ya riadha itahitimishwa Tarehe 20 Juni 2023, ikihusisha mbio za mita 200 Wasichana na Wavulana, Mita 400 Wasichana na Wavulana, Mita 3, 000 Wasichana na wavulana, zote zikitarajiwa kufanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari wavulana Tabora.

 

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…