OR – TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Angellah Kairuki amesema changamoto za wananchi ndio kipaumbele cha Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kuzitafutia ufumbuzi na kuzishughulikia kwa wakati.
Hayo yamejibainishwa mapema leo tarehe 11 Februari, 2023 Jijini Dodoma alipokutana na kuzungumza na Wabunge wa Majimbo ya Mkoa Songwe.
Waziri Kairuki amesema lengo la kuonana nao ni kuzungumzia juu ya changamoto zinazowakabili wananchi na kupata muafaka wa pamoja katika kupeleka huduma muhimu zikiwemo huduma za Utawala Bora, Elimu, Afya na Miundombinu ya barabara.
Mpaka sasa Waziri Kairuki ameshakutana na kufanya mazungumzo na Waheshimiwa Wabunge wa Majimbo ya Mikoa 17 kwa lengo la kutatua changamoto za wananchi kwenye maeneo yao.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






