BRYSON MSHANA, TABORA
Timu za Kikapu Wasichana kutoka Mkoa wa Arusha, na Dar es salaam Wavulana zimeingia hatua ya fainali katika Mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA 2023) Mkoani Tabora.
Katika michezo ya nusu fainali iyochezwa Asubuhi ya Tarehe 22 Juni 2023 kwenye viwanja A na na B vilivyopo shule ya Sekondari Tabora wavulana, Mabingwa watetezi wa UMISSETA upande wa Kikapu, Arusha waliadhibu Singida vikapu 61-24.
Mchezo mwingine wa Nusu Fainali wasichana uliwakutanisha Kilimanjaro na Dar es salaam, ukimalizika kwa Kilimanjaro kuibuka na ushindi wa vikapu 62-57 matokeo ambayo yatawakutanisha majirani Arusha na Kilimanjaro katika mchezo wa fainali.
Upande wa Kikapu Wavulana, Mwanza iliifunga Pemba 58-47,na Mabingwa watetezi Dar es salaam ikaiadhibu Arusha 64-27 hivyo fainali itawakutanisha Mwanza na Dar es salaam Jumamosi Tarehe 24 Juni 2023.
Mchezo wa Fainali ya Kikapu Wasichana na Wavulana pamoja ile ya kutafuta nafasi ya tatu, itachezwa katika viwanja A na B Shule ya Sekondari Wavulana Tabora.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






