JUMA MOHAMED, MTWARA

mtwarapressclub@gmail.co

Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko, amewataka wakazi wa Mtwara kuondoa tofauti za vyama vya siasa na kuungana katika mambo yanayowaletea maendeleo.

Dkt. Biteko amezungumza hayo leo Novemba 15, 2023 katika kijiji cha Nachenjele Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara mkoani humo, ambako amekwenda kuwasha umeme wa REA awamu ya Tatu mzunguko wa Pili.

“Kila mtu abaki na chama chake, lakini kwenye maendeleo tuungane, akifanya vizuri wa CCM nyie wa upinzani muungeni mkono mseme wewe unafanya vizuri na muwe mfano.”

“Kwamfano Mama Samia anafanya kazi nzuri hata wa upinzani mkisema anafanya kazi nzuri sio dhambi, sisi tunakuwa mfano tunamtaja Shamsia (Mbunge wa Mtwara Vijijini) hapa tukijua ni wa chama kingine lakini kwa habari ya maendeleo tunasema anafanya kazi nzuri, kama ni kuungwa mkono na mimi nawaombia mumuunge mkono.” Amesema Dkt. Biteko.

Ameongeza “Tunacheleweshana kwasababu ya kuangalia vyama, tunacheleweshana kwasababu tunachukuwa muda mwingi kuangalia chama cha mtu baadala ya mazuri yake.”

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…