BRYSON MSHANA, TABORA

mtwarapressclub@gmail.com

Timu ya Mpira wa Wavu ya Wasichana kutoka Mkoa wa Mtwara, imeanza vizuri mshindano ya ya umoja wa Michezo na taaluma kwa wanafunzi wa Shule za Mshingi Tanzania (UMITASHUMTA) kufuatia ushindi ilioupata dhidi ya Timu ya mkoa wa Tanga.

Katika mchezo uliochezwa mapema Juni 03, 2023 kwenye viwanja vya shule ya wasichana Tabora, Timu ya mkoa wa Mtwara iliibuka na ushindi wa Seti 3 – 0 na kuanza vema harakati za kutetea ubingwa katika mashindano ya mwaka huu.

Kwa upande wa mpira wa Mikono, Timu ya Mkoa wa Mtwara wasichana, imetoshana nguvu kwa kutoa sare ya 5 – 5 na timu ya Mkoa wa Iringa.

Mchezo huo wa kisisimua uliokuwa umejaa kila aina ya ufundi, ulifanyika Juni 03, 2023 katika uwanja wa shule ya Sekondandari wasichana ukishuhudiwa na viongozi mbalimbali waliopo mkoani Tabora kwa ajili ya michezo ya UMITASHUMTA.

Michezo mingine ya mpira wa mikono (Wasichana) ulizikutanisha Dodoma na Katavi zilizomaliza kwa 8-7, huku matokeo mengine yakiwa Katavi 7 Singida 20, Mbeya 9 Songwe 19, Pwani 7 Manyara 11, Mwanza 18 Arusha 9 na Rukwa 12 Kilimanjaro 9.

Kwa upande wa Mpira wa mikono Wavulana Matokeo yalikuwa Dodoma 10 Katavi 4, Iringa 14 Songwe 15, Arusha 16 Simiyu 14.

Mashindano ya UMITASHUMTA & UMISETA mwaka 2023, yanaandaliwa na kusimamiwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…