BRYSON MSHANA, MTWARA
mtwarapressclub@gmail.com
Jamii imeshauriwa kushiriki katika ufuatilaiji na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika maeneo yao.
Ushauri huo umetolewa Disemba 27,2023 na Deogratius Makoti ambaye ni Afisa ufuatiliaji wa mradi wa utekelezaji fedha za covid 19 za ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Halmashauri ya Mtwara kutoka shirika lisilo la kiserikali la MTWANGONET.
MTWANGONET ni Mtandao wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Wilaya ya Mtwara, ambalo limefanya kikao cha tathmini kilichofanyika katika ukumbi wa TCCIA Mjini Mtwara.
Dkt Makoti ameeleza kuwa pasipo ushiriki wa Wananchi katika Miradi hiyo kuna uwezekano mkubwa wa huduma kutokuwa endelevu, na isiyo kidhi vigezo vinazotakiwa na serikali kwa Wananchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashuri ya Mtwara Vijijini Selemani Nampanye amelipongeza shirika la MTWANGONET kwa kazi kubwa wanayoifanya kwani wamekuwa wakifanya kazi kama kiunganishi baina ya Wananchi na Serikali.
“Mashirika haya yanasaidia kuibua na kuonesha changamoto za kiutendaji zilizopo katika Halmashauri ambazo huenda kwa kufahamika au kuibuliwa na serikali kuzifanyia kazi” ameeleza
Naye Getrude Frank afisa Elimu kata ya Mbawala, amesema kuwa uwepo wa mashirika ya kiraia yanasaidia kuzitambua changamoto na wakati mwingine kuelekeza namna ya kutatua ikiwemo katika jamii, viongozi na serikali kwenye uwajibikaji katika shughuli za maendeleo.
Amesema kupitia shirika hilo wametambua kuwa ushirikishwaji wa jamii katika hatua za awali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao, inajenga uwajibika imara baina yao na kuondoa changamoto za baadhi ya Wananchi kutoshiriki ikiwepo kujitolea,kulinda na wakati mwingine kuipa thamani yake.
Hiki ni kikao cha tathmini ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Mradi wa fedha za COVID 19 za ujenzi wa vyumba vya Madarasa ya shule za sekondari Halmashauri ya Mtwara vijijini kupitia shirika lisilo la kiserikali la MTWANGONET, kilichohusisha wadau mbalimbali wa Elimu na viongozi wa Serikali kutoka Halmashauri ya Mtwara Vijijini.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






