MWANDISHI WETU, BUNDA
mtwarapressclub@gmail.com
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja, ametoa miezi mitatu kwa Mkandarasi anaetekeleza mradi wa maji wa Mugango-Kiabakari-Butiama ambaye ni Kampuni ya Unik Construction Engineering (UNIK) kukamilisha mradi huo kwasababu mpaka sasa wapo nyuma ya muda katika utekelezaji.
Mhandisi Luhemeja ametoa maagizo hayo akiwa katika ziara ya kikazi ya tathmini ya miradi ya maji mkoani Mara.
“Kama Serikali tunasema sasa basi, Mkandarasi inabidi kukamilisha mradi ifikapo tarehe 30 Septemba, 2023 Ili wananchi wa Mugango-Kiabakari-Butiama waweze kupata majisafi na salama” Mhandisi Luhemeja amesema.
Luhemeja ameongeza kuwa pamoja na kazi kubwa na nzuri iliyofanyika katika mradi huu, suala la muda halivumiliki tena na ikitokea Mkandarasi akishindwa kukamilisha, hatua za Kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Msimamizi wa mradi huo Mhandisi Mashaka Sita amemhakikishia Naibu Katibu Mkuu kuwa watahakikisha wanamsimamia mkandarasi ili mradi huo ukamilike, na wananchi wapate huduma ya maji.
Kwa upande wake Mkandarasi wa mradi huo, akiwakilishwa na Mhandisi Raphael Mchome ameshukuru kwa ziara ya Naibu Katibu Mkuu katika mradi huo na kuahidi kukamilisha mradi ndani ya muda uliopangwa.
“Tunamshukuru Naibu Katibu Mkuu kwa kuja Leo katika mradi huu, ujio wake umemaliza changamoto zilizotukabili na kutupa matumaini makubwa, niweze kusema tutapambana kwa kila njia ifikapo Tarehe 30 Septemba, 2023 wananchi wapate maji” Mhandisi Mchome ameahidi
Mradi wa maji Mugango-Kiabakari-Butiama unaotekelezwa kwa gharama za shilingi bilioni 70 utahusisha ujenzi wa matenki matatno (5) vituo vya kusukuma maji vitatu (3), vituo vya kuchota maji 48, mtambo wa kuzalisha maji Lita milioni 35 kwa siku, pamoja na vituo viwili vya kusukuma maji.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






