MWANDISHI WETU, KILWA

www.mtwarapressblog.co.tz

Serikali imewataka wananchi kutumia boti ya kisasa ya Utalii  ili kukuza utalii wa ndani.

Kauli hiyo ameitoa Waziri wa Maliasili na Utalii Mohamed Mchengerwa  akiwa Kilwa Masoko kwenye hafla ya uzinduzi wa  boti  maalum ya Utalii ijulikanayo kama  TAWA SEA CRUISER  inayomilikiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).

Mchengerwa amefafanua kuwa  boti hiyo itakuwa ikifanya safari katika ukanda  wote wa Pwani ili wajionee vivutio mbalimbali vya utalii.

Amevitaja baadhi ya vivutio  vya utalii vinavyopatikana  katika eneo la Kilwa kuwa ni pamoja na misitu ya matumbawe, kasa, mikoko, na samaki wa aina mbalimbali.

Katika hatua nyingine  ametembelea maeneo  ya kitalii ya mji mkongwe wa kihistoria wa Kilwa  na kujionea  vivutio vya utalii vya asili kama msikiti wa Karne ya 12  magofu ya kale na jumba la mfalme.

Akiwa katika msikiti wa kale ameiagiza Bodi ya TAWA  kuona namna ya kuboresha mji huo ili kuvuta watalii wengi.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…