MWANDISHI WETU, MANYARA
mtwarapressclub@gmail.com
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, leo Disemba 05, 2023 amewajulia hali majeruhi wa mafuriko yaliyosababisha kuporomoka kwa tope na mawe kutoka mlima Hanang, Katesh Mkoani Manyara.
Majeruhi hao wanapatiwa matibabu bure na Serikali katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa manyara, huku juhudi za uoakoaji zikiendelea kufanywa na vikosi mbalimba vya uokoaji ambavyo vimeweka kambia katika eneo lilipotokea mafuriko hayo.
Maporomoko ya tope yalitokea tarehe 03 Disemba, 2023 ambapo yalitoka mlima Hanang uliopo Mkoa wa Manyara na kusababisha vifo vya watu, majeruhi na uharibifu mkubwa wa miundombinu mbalimbali yakiwemo mashamba, na makazi ya wananchi wa eneo hilo.
Tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, ameshatoa maelekezo kwa viongozi mbalimbali kuhakikisha kuwa waathirika wote wanahudumiwa ikiwa ni pamoja na kutibiwa kwa gharama za Serikali.
Kwa upande wake Mbunge wa Hanang’ Samwel Hayuma ameipongeza serikali kwa namna inavyoendelea kuchukua hatua za haraka za kuokoa na kusaidia wahanga wa maafa hayo, huku akiwasisitiza wananchi hao kuendelea kuchukua tahadhari kwa maeneo yote yaliyoathirika na tope hilo.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






