MUSSA MTEPA, MTWARA

mtwarapressclub@gmail.com

Waislamu nchini wametakiwa kuishi katika misingi ya kumpendeza Mwenyezi Mungu na kuachana na vitendo vinavyoweza kumkasirisha.

Wito huo umetolewa  Mjini mtwara Julai 15, 2023, na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Prof Al Haji Nurdin Abdala Mangochi, wakati akizungumza mara baada ya kurejea kutokea Makkah katika Ibada ya Hijja ambapo ameseama kuwa binadamu anatakiwa kuishi vizuri na watu wanao mzunguka kwa kufuata yale yanayo mpendeza mwenyezi Mungu.

Prof. Mangochi amesema mtu yoyote aliyeenda Makkah akarudi na kufanikiwa kukubaliwa Ibada yake anahesabiwa hana dhambi hivyo sio vizuri baadae kuiharibu kwa kufanya vitendo visivyo mpendeza Mwenyezi Mungu.

“Ukienda Makkah na ibaada yako ikakubalika unakuwa huna dhambi hata kidogo kabisa unafana kabisa kama siku aliyokuzaa mama yako mtukufu, hivyo unatakiwa kuindeleza na sio kwa kipindi cha siku, mwezi au kipindi fulani ukaacha yanayompendeza Mwenyezi Mungu.” Amesema Prof. Mangochi.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…