BRYSON MSHANA, MTWARA

www.mtwarapressblog.co.tz

Siku ya Figo Duniani ni hafla ya kila mwaka ya kimataifa, inayoadhimishwa tarehe 9 Machi kila mwaka, ambayo inalenga na kulenga kuongeza uelewa juu ya umuhimu wa afya ya figo na kupunguza kiwango cha maambukizi duniani.

Siku hii ilianza kuadhimishwa rasmi mwaka 2006 katika nchi 66 na baadae kuenea katika nchi zote duniani, huku nchini Tanzania siku hii ilianza kuadhimishwa mwaka 2011.

Lengo la kuadhimisha siku hii ni kufanya kampeni ya kidunia inayolenga kuongeza ufahamu kwa watu juu ya umuhimu wa figo na kuwahamasisha kuchukua tahadhari ya kujikinga dhidi ya maradhi ya figo (magonjwa sugu ya figo) na matatizo mengine ya kiafya yanayohusiana na figo.

Mwaka huu, mada ya Siku ya Figo Duniani 2023 ni Afya ya Figo kwa Wote—Kujitayarisha kwa ajili ya yasiyotazamiwa, Kutegemeza Walio hatarini!” ambayo inasisitiza umuhimu wa kutambua mapema ugonjwa wa figo, usimamizi bora na utunzaji.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Lishe Tanzania, Magonjwa sugu ya figo ni moja wapo ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo pamoja na sababu nyingine yanayohusiana pia na ulaji usiofaa na mitindo ya maisha isiyosahii.

Magonjwa haya huingia katika mwili wa binadamu kimya kimya bila ya kuonesha dalili za awali, na dalili hujitokeza ugonjwa ukishakomaa aidha katika hatua ya kwanza na kuendelea.

Taarifa ya Taasisi hiyo inaeleza kuwa ni vyema kila mmoja akajenga tabia ya kufanya uchunguzi wa figo mara kwa mara na kufuata ushauri wa wataalamu.

Kulingana na tafiti, mtu mmoja kati ya kumi anaugua ugonjwa wa figo, huku sababu kuu za hatari kwa ugonjwa wa figo ni pamoja na shinikizo la damu, kisukari, fetma na historia ya familia ya ugonjwa wa figo.

Ugonjwa wa figo pia unaweza kusababishwa na magonjwa ya kinga mwili, maambukizo, na matumizi mabaya ya dawa za kulevya.

Kulingana na hali hiyo, kamati kuu ya siku ya figo duniani (WKD) inaitaka jamii sio tuu kuwa na muamko wa magonjwa ya figo, bali pia kufanya vipimo ili kujua hali ya figo zao.

Hii ni pamoja na kujua kiwango cha shinikizo la damu lipo ngapi na malengo ni kutaka lifike ngapi.

Kamati hiyo inasema kuwa malengo ya kupambana na ugonjwa figo yanapaswa kuungwa mkono na watu wote zikiwepo jumuiya za mambo ya figo ulimwenguni, madaktari, wanasayansi, wauguzi, wahudumu wengine wa afya, wagonjwa, watawala, wataalam wa sera na watumishi wa kiserikali.

Kwa mujibu wa Daktari ingwa wa Figo Mercy Julian anaeleza kuwa ili kujikiga a ugojwa wa Figo inafaa kula chakula ora, matunda samama a kujitahidi kuywa maji lita moja a nusu hadi mili kwa siku.

Vilevile anatahadharisha kuwa dalili zingine za ugonjwa wa figo ni kuvima macho na miguu, kuawa na kifua (kukohoa) pamoja na kuwashwa mwili.

Mwaka 2022, Takwimu za Shirika la Afya Dunniani (WHO) zilionesha kuwa wastai  asilimia 10 ya watu wote dunianni wannaishi a ugojwa sugu wa figo huku asilimia 11 hadi 17 ya watu waansoisha kusini mwa jangwa la sahara wakielezwa kuwa na ugonjwa huo.

Nchini Tanzania utafiti ulibaini kuwa takribani watazania 5,800 mpaka 8,500 waahitaji huduma ya kusafisha damu au kupandikiza figo na hadi kufikia January 2022 wagonjwa 2,750 sawa na asilimia 32 walipata huduma ya kusafisha damu na wengine 325 walipandikizwa figo.

Kati ya waliopandikizwa Figo, 93 walifanyiwa huduma hiyo hapa nchini, hospitali ya Taifa ya muhimbili ikipandikiza wagonjwa 67 na Benjamin mkapa ya dodoma wagongwa 26.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…