Na Mwandishi wetu, Kilimanjaro
Tanzania imeendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa inaendelea kuitangaza lugha ya Kiswahili katika maeneo mbalimbali Duniani kupitia utalii.
Kwa mujibu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, lengo la zoezi hilo lililofanyika tarehe 9 Decembe 2022, ni kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili inawafikia wageni mbalimbali.
Kufuatia juhudi hizo, wananchi na wadau mbalimbali zaidi ya 200 wameshiriki maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru wa Tanganyika kwa kupanda mlima Kilimanjaro,Wizara ya Elimu, zoezi lililoenda sambamba na kauli mbiu ya “Twende zetu kileleni”
Zoezi la upandaji wa Mlima Kilimanja limelenga kukipeleka Kiswahili kileleni, kuashiria kuwa lugha hiyo inamulika mataifa ya nje ya mipaka ya Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Burundi Jilly Maleko, ni mmoja wa washiriki wa zoezi hilo ambaye amesema kuwa Burundi tayari wanaongea Kiswahili lakini bado wanahitaji kujengewa uwezo zaidi katika nyanja za ufundishaji.
Ameeleza kuwa tayari makubaliano yameshaingiwa kati ya Tanzania na Burundi ili kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili inafundishwa katika vyuo na shule za sekondari nchini humo.
“Tumejizatiti katika kukikuza Kiswahili katika nchi nyingi duniani, kwa upande wa Burundi tayari tumeshaanza kutekeleza makubaliano ya kufunsisha Kiswahili katika chuo kikuu na shule za sekondari hatua ambayo naweza kusema ni kubwa” ameeleza Balozi Maleko
SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI USHIRIKI WA WADAU KATIKA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI
Na Munir Shemweta Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ushiriki wa wadau katika…






