MWANDISHI WETU, ZANZIBAR

mtwarapressclub@gmail.com

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kitaifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, ameongoza kikao cha Kumi cha Kamati hiyo kilichofanyika katika tarehe 15 Januari, 2024.

Kikao hicho kimefanyika kwenye  Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar, kikihudhuriwa pia na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Mhe. Hemed Suleiman Abdulah ambaye ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati hiyo.

Viongozi wengine walioudhuria ni Mawaziri wa kisekta wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Makatibu wakuu wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi

Sensa ya watu na Makaazi ilifanyika nchini Tanzania mwezi Agusti 2022.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…