BRYSON MSHANA, MTWARA
www.mtwarapressblog.co.tz
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmedi Abbas Ahmedi, amekutana na waandishi wa habari Ofini kwake leo Julai 27, 2023 kwa ajili ya kutoa taarifa ya maandalizi ya maonesho ya nanenane Kanda ya Kusini yanayotarajiwa kuanza rasmi Agusti 01, 2023 kwenye viwanja vya Ngongo vilivyopo Manispaa ya Lindi.
Katika Mkutano huo, Kanali Ababas ameeleza kuwa tayari miundombinu ikiwepo ya barabara imeimarishwa kwa kiwango cha lami katika viwanja vya maeonesho, sambamba na usambazaji wa umeme na maji.
Amewataka wananchi wa Mikoa ya Mtwara, Lindi na maeneo ya jirani kujitokeza kwa winging kwenye maonesho ya Nanenane 2023, yanayotarajiwa kujumuisha washiriki zaidi ya 500 ambao ni sawa na ongezeko la asilimia 36 ikilinganishwa na washiriki 369 wa Nanenane ya mwaka 2022.
“Mwaka huu kumetengwa siku nne maalum kuanzia tarehe 3 hadi 7 Agusti 2023, ambazo zitazingatia kwenye kuhamsisha utalii na uhifadhi wa mazingira, kuhamasisha siku ya ya ulaji wa bidhaa za Korosho, kuhamasisha ulaji wa vyakula vya asili na matumizi ya mbegu za asili, na kuhamasisha ulaji wa bidhaa za mifugo na viumbe vya baharini” ameeleza Kanali Ababas
Ameongeza kuwa maonesho ya mwaka huu pia yatajumuisha ufundishwaji wa Teknolojia mbalimbali zinazochangia kuongeza uzalishaji na tija kwenye eneo la umwagiliaji kwa njia za matone ,usindikaji wa mazao , malisho ya mifugo , ufugaji wa samaki na viumbe wa baharini kiwemo majongoo ya bahari “
Kwa upande wake Mshauri wa Kilimo Mkoa wa Mtwara Bwana Ali Linjenje, amekitaja kilimo cha Mwani na ufugaji wa Majongoo ya bahari kama moja ya mambo ambayo yameshika kasi hivi sasa, akieleza vyote vitatolewa elimu wakati wa meonesho ya Nanenane 2023 Kanda ya kusini.
Naye Bi. Nanjiva Godfrey Nzunda Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Mtwara, amesema tayari kumeonekana kuwa na uhitaji mkubwa wa mazao ya bahari, hivyo kupitia maonesho ya nanenane wataendelea kutoa elimu kwa wafugaji wa na wakulima ili waweze kufaidika zaidi.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






