BRYSON MSHANA, MTWARA

mtwarapressclub@gmail.com

Wananchi mkoani Mtwara wametakiwa kutofumbia macho na badala yake wakemee na kuripoti vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyotokea katika maeneo yao.

Wito huo umetolewa Novemba 25 ,2023 na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mwanahamisi Munkunda,wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ufunguzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia  kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas .

DC Mwanahamisi ameeleza kuwa vitendo vingi vya ukatili wa kijinsia vinaanza na kuenea katika maeneo watu wanapoishi, hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha kuwa anatumia nafasi yake kukomesha hali hiyo ili jamii iendelee kuwa salama.

“Ukiwa kama Mzazi ukiwa kama Mwana jamiii ukisikia mtoto wa mwenzio kalawitiwa au kabakwa ujue pia familia yako haiko salama kwasababu mzunguko huo utazidi kukua” amesema Mkuu wa Wilaya

Mkuu wa wilaya amewaomba wadau yakiwepo mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojishughulisha na kupinga ukatili wa kijinsia, waendelee  kutoa elimu  kwa jamii juu ya athari za vitendo hivyo ili kuendelea kuokoa jamii.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Shirika la FAWOPA Balthazar Komba, amesema kuwa wamejipanga kupita katika maeneo mbalimbali mkoani mtwara, ili kuwafikia wananchi na kuwapa elimu yuu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Kampeni ya siku 16 za kupinga Ukatili mkoani Mtwara imeandaliwa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mtwara chini ya Mtandao wa MTWANGONET kwa kushirikiana na Ofisi ya Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mtwara, huku kauli mbiu ya mwaka 2023 ikiwa ni “Wekeza Kuzuia Ukatili Wa Kijinsia”

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…