MWANDISHI WETU, KIBAHA

mtwarapressclub@gmail.com

MKUU wa Mkoa wa Pwani Alhaj Aboubakar Kunenge amehimiza ushirikiano baina ya Taasisi za Umma, Binafsi na watendaji kwenye Halmashauri ili kazi ya kuwatumikia wananchi iwe rahisi.

Ameyasema hayo Machi 30, 2023 wakati  akifungua semina ya kujenga uelewa wa shughuli za taasisi mbalimbali za umma na binafsi ikiwemo Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) na watendaji kutoka Halmashauri za Mkoa wa Pwani 

GBT ni taasisi ya Kiserikali ambayo iko chini ya Wizara ya Fedha na Mipango ikisimamiwa na Msajili wa Hazina. (TR).

RC Kunenge amesema wataalamu lazima wajue viongozi wa kisiasa hawawezi kuwa na maamuzi mazuri kama wataalamu hawatafanya kazi ya kitaalamu inavyotakiwa.

 “Lazima tuelewe, serikali ni moja, mlipaji ni mmoja, fedha inatoka fungu moja na inavyopatikana iwe ni
Halmashauri au Bodi ya Michezo ya kubahatisha yote inaingia sehemu moja kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha au PST.” 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Bw. James Mbalwe
amesema Bodi imefika Mkoani humo kwa lengo la kujitambulisha rasmi kwa watendaji wa Mkoa ili kuongeza ufahamu wa kamati, uwepo wa taasisi na kuongeza ufahamu juu ya usimamizi na uendeshaji wa michezo ya kubahatisha hapa nchini.

Pia kuimarisha ushirikiano katika usimamizi na udhibiti wa sekta na kuomba kamati ya Ulinz na Usalama
ya Mkoa kushirikiana na GBT ili kudhibiti wavunjaji wa sheria ya michezo ya kubahatisha hapa mkoa wa Pwani, ame sema Bw. Mbalwe.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…