mtwarapressclub@gmail.com
Jopo la majaji katika kesi ya madai limempata Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump n ahatia ya kumnyanyasa kingono mwandishi wa jarida katika duka moja kuu la New York miaka ya 1990.
Hii ni mara ya kwanza kwa Bw Trump kupatikana na hatia ya kuhusika na unyanyasaji wa kingono, lakini hakupatikana na hatia ya kumbaka E Jean Carroll katika chumba cha kubadilishia nguo cha Bergdorf Goodman.
Mahakama pia ilimpata Bw Trump na hatia ya kuharibia jina kwa kuyaita madai ya mwandishi huyo “Uvumi na uwongo”.
Mahakama ya Manhattan iliamuru Bw Trump amlipe takriban dola milioni milioni tano kama fidia.
Jopo hilo la majaji tisa ilifikia uamuzi wao baada mashaurinao ya chini ya saa tatu siku ya Jumanne.
“Leo, ulimwengu hatimaye unajua ukweli,” Bi Carroll alisema katika taarifa iliyoandikwa kufuatia uamuzi huo.
“Ushindi huu sio kwangu tu bali kwa kila mwanamke ambaye ameteseka kwa sababu hakuaminiwa.”
Wakili wa Bw Trump alisema rais huyo wa zamani anapanga kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI USHIRIKI WA WADAU KATIKA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI
Na Munir Shemweta Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ushiriki wa wadau katika…






