Spika wa Bunge Tanzania, Dkt. Tulia Ackson ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kundi la Afrika katika Umoja wa Mabunge Duniani (Africa Geopolitical Group in the IPU), Machi 10, 2023 ameongoza Kikao cha Kundi la SADC katika Umoja wa Mabunge Duniani (SADC Geopolitical Group in the IPU).
Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Paddock 6, Bahrain International Circuit (BIC), Manama, Bahrain kabla ya kufunguliwa kwa Mkutano wa 146 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).
Katika mkutano huo, Mhe. Dkt. Tulia ameambatana na Wabunge Wawakilishi wa Bunge la Tanzania kwenye Umoja huo ambao ni Dkt. Joseph Mhagama, Elibariki Kingu, Mhandisi Mwanaisha Ulenge, Ramadhan Ramadhan, Dkt. Faustine Ndugulile pamoja na Katibu wa Bunge Ndg. Nenelwa J. Mwihambi,

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






