MTWARA

Chama cha Waalimu Manispaa ya Mtwara kimefanya mkutano wake mkuu ulioambatana na zoezi la uchaguzi kwa ajili ya kuwapata viongozi mbalimbali watakaokiongoza Chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano Ijayo.

Mwenyekiti wa Chama Cha Waalimu Mkoa wa Mtwara Mwalimu ndule Emanuel ameelezea Mkutano huo kuwa ni wa kikatiba na umewapa fursa wajumbe kuwachagua viongozi watakaowatumikia katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa CWT Mkoa wa Mtwara, ambapo Mwalimu Mayunga Jetinya amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho katika Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Akizungumza baada ya uchaguzi huo Mwalimu Matinya amewashukuru wajumbe waliomchagua, huku akiahidi ushirikiano na kuendelea kuwaunganisha waalimu ili wazidi kuwa wamoja na kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili.

“Katika kipindi cha uongozi wangu nitaenda kuyalinda na kutetea maslahi ya waalimu lakini katika hilo lazima tushirikiane pamoja na kushirikisha Taasisi zingine”

Uchaguzi huu wa Mtwara Manispaa unahitimisha zoezi la uchaguzi katika Wilaya za Mkoa wa Mtwara na sasa kinachosubiriwa ni uchaguzi wa ngazi ya Mkoa kulingana na ratiba itakavyopangwa.

Check Also

SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI USHIRIKI WA WADAU KATIKA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI

Na Munir Shemweta Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ushiriki wa wadau katika…