MWANDISHI WETU – DODOMA
mtwarapressclub@gmail.com
Uongozi wa Benki ya NMB umeahidi kuendelea kuunga mkono shughuli za Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu katika kuhakikisha wanaimarisha uhusiano uliopo na kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuratibu shughuli za Serikali.
Hayo yameelezwa Februari 08, 2024 na Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa Serikali na Ofisi ya Makao Makuu Ndogo ya NMB- Dodoma, Bi Vicky Bishubo wakati walipotembelea na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Jim Yonazi pamoja na Naibu wake Bw. Anderson Mutatebwa ofisini kwake Jijini Dodoma.
Bi Vicky amesema kuwa, katika kutoa huduma za kibenki ambazo zinahusu ofisi ya Waziri Mkuu wataendelea kuyafikia makundi mbalimbali ikiwemo vijana kwa kutoa huduma za kibenki popote walipo na hii itasaidia kusukuma juhudi za Serikali katika huduma za kifedha.
“Tumeendelea kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, na hii haitokuwa mwisho tunaahidi kuendelea kufanya hivyo katika kuunga mkono shughuli mnazotekeleza,” amesema Vicky
Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amesema kuwa, Benki ya NMB imefanya jambo muhimu kuitembelea ofisi yake na kueleza namna ilivyojipanga kuhakikisha inaunga mkono shughuli za Serikali na kuwasihi waendelee kufanya hivyo kadiri inavyofaa.
“Ninawapongeza NMB kwa moyo huu na mmetupa kuona umuhimu wa kuimarisha umoja uliopo nitoe wito muendelee kutoa huduma bora za kibenki kwa jamii yetu ili wananchi waendelee kunufaika na uwepo wenu na kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla,” amesema Dkt. Yonazi
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Anderson Mutatebwa aliwashukuru NMB kwa kuitembelea ofisi hiyo na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo bana yao.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






