MWANDISHI WETU, MOROGORO

mtwarapressclub@gmail.com

Baraza la Taifa la Watu wanaishi na Virusi vya ukimwi (NACOPHA), limetangaza uongozi wake huku Mwenyekiti wake Leticia Kapela akisisitiza juu ya kufanya shughuli za uzalishaji ili kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza Mjini morogoro Novemba 29, 2023 katika sherehe ya kiapo baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo, Mwenyekiti Leticia Kapela alisisitiza haja kwa watu wanaoishi na UKIMWI kutoka kwenye utegemezi, akiwaomba kujihusisha kikamilifu katika shughuli za ujasiriamali.

“Jamii yetu lazima iache utegemezi na   ichukue hatamu za ujasiriamali kama njia ya kufikia kujitegemea kiuchumi,”

“Tunaamini kwamba kwa kuchochea ujasiriamali, tunaweza kuwawezesha watu kuishi maisha yenye maana na ya kujitegemea,” ameongeza Mwenyekiti Kapela.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa NACOPHA Ndugu Deogratias Rutatwa, ameelezea malengo ya kimkakati yaliyowekwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanashirikiana na serikali katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali.

Rutatwa ametumia nafasi hiyo kuishukuru serikali za Tanzania na Marekani, kupitia mashirika ya PEPFAR na USAID, kwa mchango wao mkubwa kwa miradi ambayo imekuwa ikitekelezwa na NACOPHA, ukiwepo mradi wa “HEBU TUYAJENGE.”

“Msaada thabiti kutoka kwa serikali za Tanzania na Marekani umekuwa muhimu katika juhudi zetu za kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya wale wanaoathiriwa na UKIMWI, kupitia mradi wa ‘HEBU TUYAJENGE,’ tunalenga kujenga jamii imara inayofanikiwa kupitia ujasiriamali,” amesema Deogratias Rutatwa.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…