RAMLA MASALI, MTWARA

mtwarapressclub@gmail.com

Mtoa Mada kutoka katika Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Deogratius Temba amesema Mila na Desturi za Unyago, inakwamisha baadhi ya wanawake walio wengi hasa kwa upande wa Kusini kushiriki katika masuala ya uongozi.

Amezungumza hayo Juni 20 wakati wa kufunga Mafunzo ya kujengewa uwezo juu ya masuala ya Jinsia kwa Waandishi wa Habari 30, yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Chama cha Walimu, Tanzania, Mkoa wa Mtwara

“Mila za Jando na unyago  ni nzuri lakini inakua mbaya ndani yake kwa sababu ya mafundisho yanayotolewa kwa watoto wayafanye wakati sio muda sahihi  kwao , sana sana yanawaathiri katika makuzi yao na kujiona dhaifu hivyo wanshindwa kushiriki hata masuala ya uongozi “ amesema Deogratius

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Karim Faida ,Mkurugenzi wa Faida Tv, amesema mafunzo hayo yamewasaidia kuwakumbusha  kuandika habari zenye mrengo wa kijinsia na kuelimisha jamii juu ya mitazamo hasi dhidi ya Mwanamke

“kuna misemo ambayo sio mizuri kutumia inamdidimiza mwanamke kama we ni mwanamke tu si chochote, mwanamke kazi yake kulia lia tu hii ni baadhi ya misemo ambayo jamii inatakiwa iachane nayo kwasababu wanawake wanaweza “ amesema  Faida.

Naye Bi Zam Zam Jambia Mwandishi wa Habari wa Redio Ahmadiya, amesema Mafunzo alilyoapata yatamsaidia kufanya kazi zake kwa ufanisi hasa kuandaa vipindi vinavyotoa hamasa kwa wanawake  wajitokeze kwa wingi ili wagombee nafasi za uongozi ili kuleta usawa katika Jamii.

Mafunzo hayo ya siku mbili kuanzia  Juni 19 na Juni 20 , 2023  yameandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na Chama cha waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara.

Check Also

SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI USHIRIKI WA WADAU KATIKA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI

Na Munir Shemweta Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ushiriki wa wadau katika…