MWANDISHI WETU, MANYARA
mtwarapressclub@gmail.com
Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang wameishukuru Serikali kutokana na juhudi kubwa iliyozifanya katika urejeshaji wa hali na misaada ya kibinadamu iliyotolewa kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope na mawe kutoka Mlima Hanang.
Wananchi hao wametoa shukrani zao tarehe 20 Disemba, 2023, wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama alipokagua kujionea hatua za urejeshaji wa hali katika maeneo yaliyoathirika katika Halmashauri ya wilaya ya Hanang.
Akitoa shukrani kwa Serikali Mchungaji Martine Tarimo, amesema kuwa wamefarijika kwa jinsi Serikali inayoongozwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ilivyoratibu zoezi la urejeshaji wa hali kwa waathirika wa maafa yaliyotokea Wilayani humo na kuahidi wataendelea kuunga mkono jitihada zinazochukuliwa na Serikali katika kusaidia waathirika wa maafa hayo.
“Tumeona msaada wa Serikali tangu siku ya kwanza ya madhila ya Maporomoko ya Mawe na Matope, serikali imekaa na sisi na imetusikiliza na hoja tulizotoa zimefanyiwa kazi kwa wakati,” alifafanua Mchungaji Tarimo
Akizungumza kuhusu urejeshaji wa hali, Mkazi wa Katesh Bw, Ibrahim Mwenda alisema kwa hatua hiyo wataendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha wanarejea katika hali zao za awali huku akiendelea kuishukuru Serikali.
“Tunaomba sisi kama wafanyabiashara tusiendele tena kufanya shughuli zetu hapa, tunaomba tupelekwe eneo jingine rafiki kwa shughuli zetu,” aliomba.
Naye Mkazi wa Kijiji cha Gendabi Bi. Julian Masay ameishukuru serikali kwa ufuatiliaji wa kila siku hasa katika kipindi hiki ambacho wamekubwa na madhila ya Maafa na kueleza wameendelea kupata faraja kwa namna Serikali na wadau mbalimbali walivyojitokeza katika kusaidi hilo.
SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI USHIRIKI WA WADAU KATIKA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI
Na Munir Shemweta Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ushiriki wa wadau katika…






