MWANDISHI WETU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama pamoja na Afisa habari wa Ofisi hiyo Bw. Tegemeo Kastus wameenda Katesh Hanang’  Mkoani Manyara, kufuatia maafa yaliyosababishwa na mafuriko yaliyotokea Asubuhi ya Disemba 3, 2023.

Wengine walioambatana nao ni kikosi cha pili cha Jeshi cha uokoaji, kuelekea kwenye tukio kwa ajili ya kuendelea na zoezi la uratibu uokoaji katika eneo hilo.

Inaariwa kuwa zaidi ya watu 20 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa, kufuatia mafuriko yaliyosabishwa na mvua zinazoendelea kunyesha Wilayani Hanang’ mkoani Manyara.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…