MWANDISHI WETU, LINDI
mtwarapressclub@gmail.com
Watu 14 wamefariki dunia na wengine 26 kujeruhiwa katika ajali ya Basi lenye namba T 336 DPW la kampuni ya Baraka, lililoanguka kitongoji cha Mputo kata ya Mtama mkoani Lindi.
Akitoa taarifa rasmi ya ajali hiyo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) John Imori, amesema taarifa za awali zinaonesha kuwa chanzo cha ajali ni hitilafu ya breki ya Basi hilo, iliyopelekea dereva kushindwa kuhimili.
“Dereva alibaini kwamba gari lina hitilafu ya breki lakini akaendelea kuendesha na majeruhi wametueleza hivyo, na hata wananchi ambao wapo kwenye eneo hili la tukio wamethibitisha hivyo, kwahiyo dereva anatibiwa pale Nyangao na yupo chini ya ulinzi kwa hatua zaidi ya kisheria.” Amesema Kamanda Imori.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack ameagiza kuanza ukaguzi wa magari kabla ya kuanza safari ili kubaini magari yenye hitilafu, jambo ambalo litasaidia kuepuka ajali zitokanazo na ubovu wa vyombo vya usafiri.
Baadhi ya majeruhi wanaopatiwa huduma Hospitali ya Nyangao wamesema “Baada ya gari kupinduka wakaja kutuvamia na Nyuki hapohapo kwahiyo watu wakashindwa kuja kutokoa kwa haraka.” Amesema Arafa Mwashuhuli.
Mganga wa zamu Hospitali ya Nyangao, Dk. Ashanery Komba, amesema “tulipokea majeruhi takribani 26 ambao walifika hospitalini kwetu na vifo kama 14, kati yao wakiwa wanaume na wanawake lakini pia na watoto..”
“hali zao kwa majeruhi ambao tunao hapa tulikuwa na majeruhi ambao walikuwa kwenye hali mbaya zaidi ulilinganisha na wengine, wengine wamepatiwa matibabu na wameenda nyumbani lakini wale wachache kama wawili watatu wamepata majeruhi makubwa kidogo mmoja tumemlaza kwenye uangalizi wa karibu..” Amesema Dk. Komba.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






