KHOMEIN TV, LINDI
mtwarapressclub@gmail.com
Watu kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha kufuatia ajali ya Basi la kampuni ya Baraka lenye namba za usajili T 336 DPW lililokuwa linatoka wilayani Newala kuelekea Dar es Salaam, kuanguka eneo la Mtama, halmashauri ya Mtama mkoani Lindi.
Ajali hiyo imetokea leo Novemba 26, 2023 majira ya asubuhi, ambapo taarifa za awali ambazo zimetufikia ni kwamba eneo ambalo basi hilo limeanguka ni Barabara ya Mtama-Newala, karibu na daraja la Mto Lukuledi, ambako kuna kona kali kabla ya kulifikia daraja hilo.
Akizungumza kwa njia ya simu, Diwani wa kata ya Mtama, Maria Petronyale, amesema zoezi linaloendelea kwa sasa ni la uokoaji wa watu ambao bado wamo ndani ya Basi, na kwamba wale ambao walikuwa nje wamewahishwa hospitali ya Nyangao.
“Unakuja Barabara ya kwenda Newala, ukishatoka hapo Mtama Mjini, ukishaingia hii Barabara unapita kiwanda cha Korosho unapita Daraja la Mto Lukuledi, mbele yake hapa kuna sehemu ina kona mbaya sana.”
Amesema zoezi la uokojai lilikabiliwa na changamoto ya Nyuki ambao walitimka eneo ambalo Basi limeanguka, kabla ya jitihada kufanyika na kuwadhibiti.
“Lakini baadae Polisi walikuja walijitahidi kuchukuwa baadhi ya matairi mengine wakawasha moto na wakanunua Rungu hivi wakawagawia watu wakawa wanapuliza kila mtu anapuliza hapo kidogo hali ikawa imetulia, sasaivi Nyuki hawapo wametulia wapo huko kwenye maoneo yao lakini kwa hapa zoezi linaendela hapana Nyuki kwa sasa.” Ameeleza Diwani Maria.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






