BRYSON MSHANA, MTWARA

mtwarapressclub@gmail.com

Zaidi ya Tani elfu 12 za Korosho zimeuzwa kwenye manda wa Chama kikuu cha Usiririka Masasi-Mtwara-Nanyumbu (MAMCU LTD)  uiofanyika Octoa 27, 2023 katika kijiji cha Madimba Hamashauri ya Wilaya ya Mtwara Mkoani Mtwara.

Bei iliyofikiwa na wanunuzi katika mnada huo wa pili msimu 2023/2024 uliohudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mwanahamis Munkunda, ni Shilingi 2,070 kwa kilo moja, ambayo ni bei ya juu, huku bei ya chini ikiwa shilingi 1,920

Jumla ya kampuni 52 ziliwasislisha maombi ya kutaka kununua korosho zilizohifadhiwa katika maghala mbalimbali ya Mtwara,Masasi na Nanyumbu.

Akizungumza na wakulima kwenye mnada huo, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mwanahamis Munkunda amewapongeza wanunuzi waiojitokeza kununua Korosho ya Tanzania msimu 2023/2024 akisema hiyo ni ishara njema ya kukubalika kwa Tanzania katika biashara za kimataia.

“ Nawapongeza sana wanununzi hawa kupitia kampuni zao ambazo nimesikia hapa kuwa ni zaidi ya 100 wametoka katika maeneo mbalimbali duniani, hii inawaongezea nafasi ya kuendelea kuja nchini kwetu kuwekeza kwenye sekta nyingine” amesema Mkuu wa Wilaya

Amewahimiza wakulima ktunza vizuri kurosho zao wanazovuna ili ziendelee kukidhi vigoezo vinavyotakiwa, ili ziendelee kuvutia wanunuzi ambao wanafuata ubora wa Korosho zinazozalishw a Tanzania.

Kwa upande wake muwakilishi kutoka Bodi ya Korosho Tanzania Bw. Revelian Ngaiza ambaye ni Mkurugenzi wa Masoko na Udhibiti Ubora, amewataka wakulima kuendelea kuzifuatilia taarifa za hali ya masoko duniani ambazo zimekuwa zikiwasilishwa minadani kupitia wataalam mbalimbali.

Ngaiza amewaeleza Wakulima kuwa Serikali kupitia Bodi ya Korosho inaendelea kutekeleza jukumu lake la kuhakikisha kuwa inafuatilia mwenendo wa bei za Korosho zinavyoenda katika maeneo tofauti duniani, na kuziwasilisha kwa wakulima wake.

“Tupo kwa ajili ya kumlinda Mkumlima, na hilo ni pamoja na kuhakikisha kuwa anapata bei nzuri ya Korosho, ndio maana hata takwimu za makampuni yaliyojitokeza kutaka kununua Korosho zetu imeendelea kuongezeka hadi kufikia 103, hii inaonesha njia njema ya Serikali katika biashara hii ya Korosho” amesisitiza Ngiaza

Akizungumza baada yam nada huo, Meneja wa MAMCU Biadia Matipa, amesema kuwa wanaendelea kufuatilia mwenendo wa Soko Korosho katika maendeo mbalimbali, ili wakulima wauze wakiwa wanazingatia uhalisia ya soko lilivyo duniani.

Amesema kuwa wanaendeea kufuatilia mwenendo wa soko na bei ya Korosho katika maeneo mbalimbali duniani, ili kuendeea kuhakikisha kuwa wakulima wanauza Korosho kwa bei halisi.

“Tupo kwa ajili ya kuwasimamia wakulima, moja ya majukumu yetu ni kuhakikisha kuwa wakulima wanapata bei nzuri ya Korosho kwa kipindi chote cha msimu” amesisitiza Biadia

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…