MWANDISHI WETU, BABATI
mtwarapressclub@gmail.com
Taasisi ya Utalii ya chemchem iliyoko wilaya ya Babati mkoa wa Manyara, imeanza kugawa Baiskeli bure kwa Watu wenye ulemavu wa miguu zaidi ya 300 mkoani Manyara ili ziwasaidie kufanya shughuli za kiuchumi.
Baiskeli hizo, zenye thamani ya zaidi shilingi milioni 45 zimetolewa na Taasisi ya kimataifa ya Weelchair Fondation, kupitia Taasisi ya chemchem association ambayo ipo chini ya Mwekezaji wa shughuli za Utalii na uhifadhi katika eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Jamii ya Burunge wilaya ya Babati.
Mkuu wa wilaya ya Babati, Lazaro Twange akizungumza wakati wa kukabidhi baiskeli hizo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga, amesema msaada huo ni kwa ajili ya watu wenye ulemavu ambao wanaishi katika vijiji vinavyounda hifadhi ya eneo la hifadhi ya jamii ya Wanyamapori ya Burunge alipongeza Chemchem kwa msaada huo.
Twange amewataka wananchi wa mkoa wa Manyara, kuendeleza uhifadhi wa mazingira ili kuvutia watalii na wawekezaji kutoa misaada zaidi.
Amesema msaada wa Baiskeli hizo ni ishara ya mahusiano mazuri baina ya wananchi na mwekezaji wa Chemchem katika eneo hilo, kwani pia amekuwa akitoa misaada katika sekta nyingine, ikiwepo elimu, Afya na Maji.
“Nawaomba tuendekeze mahusiano haya mazuri ili tupambane na matukio ya ujangili katika eneo letu ili tuvutie watalii zaidi ambao wataleta fedha ambazo zitaendelea kugawanywa vijiji 10 vinavyounda Burunge WMA”amesema
Alisema Baiskeli hizo zisaidiwe wenye ulemavu kuweza kushiriki vyema shughuli za kiuchumi na kujiletea maeneo.
Naye Mkurugenzi wa Chemchem Association, Fabia Bausch amesema wanajivunia uwepo wa mahusiano mazuri na jamii na ndio sababu wataendelea kutoa misaada mbalimbali kusaidia kijamii.
Amesema licha ya msaada huo wa Baiskeli pia wanaendelea kusaidia pia makundi ya akina mama kujikwamua kiuchumi kwa kupewa fedha na elimu ya ujasiriamali,kusaidia vita dhidi ya ujangili na wamesaidia ufadhili wa masomo kwa wanafunzi.
“Tumekuwa tukisaidia miradi ya elimu,maji Afya lakini pia kuwasaidia akina mama kushiriki vyema katika Utalii”amesema
Akizungumza kwa niaba ya wanufaika wa Baiskeli hizo, Maria Haido ameishukuru taasisi ya chemchem na Serikali kufanikisha kupatiwa Baiskeli na kuahidi sasa ataweza kutoka nyumbani na kwenda kujitafutia mahitaji yake kwa urahisi.
Meneja miradi wa Taasisi ya Chemchem association,Martin Mng’ongo amesema wanatarajia kugawanya zaidi ya Baiskeli 300 mkoani Manyara na maeneo mengine yenye uhitaji.
“Leo tumeanza kutoa Baiskeli kwa baaadhi ya wenye ulemavu wanaoishi vijiji vilivyopo ndani ya Burunge WMA, ikiwa pia ni sehemu ya uzinduzi wa tamasha la chemchem 2023 na tutaendelea kutoa Baiskeli maeneo mengine”ameeleza.
Eneo la Burunge WMA lipo kati kati ya hifadhi za Taifa za Tarangire na Manyara ambapo kuna idadi kubwa ya wanyama hasa Twiga hata hivyo, kumekuwepo matukio ya ujangili wa Twiga kwa ajili ya kitoweo.
Hata hivyo,katika.siku za karibuni kumekuwepo na operesheni kubwa za kuwasaka majangili kwa kuhusisha kikosi Maalum Cha Mamlaka ya wanyamapori (TAWA) askari wa Burunge WMA na Askari wa chemchem na majangili kadhaa wamekamatwa.
SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI USHIRIKI WA WADAU KATIKA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI
Na Munir Shemweta Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ushiriki wa wadau katika…






