ALEX SONNA,DODOMA

mtwarapressclub@gmail.com

MWENYEKITI  wa Bodi ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mwantumu Mahiza,amezitaka taasisi mbalimbali  nchini kuhakikisha zinatunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Mahiza ametoa maelekezo hayo leo Oktoba 3,2023 jwakati wa zoezi la upandaji miti liliofanyika Shule ya Sekondari Ilazo Extension jijini Dodoma.

Amesema jamii inatakiwa kuhamasika katika utunzaji wa mazingira ikiwepo kupata hewa safi pamoja na Mvua zakutosha kuzalisha chakula.

“Tumekuja hapa kupanda miti kwa lengo kuhihamasisha jamii suala la kutunza mazingira sio la Serikali au Kikundi cha watu fulani ni jukumu letu sote tujitoe tutunze mazingira yetu” amesema Mwantumu

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Green Eco Tanzania Stanley Shibuda amesema Shirika hilo linahamasisha upandaji wa miti kwa nchi nzima na kwasasa limeanza kwa Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kupanda miti 1500 na mpaka sasa wamehamaisha kupanda miti 300.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…